AZAM FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR MABAO 2-1 - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 21 May 2022

AZAM FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR MABAO 2-1


 AZAM FC leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa mzunguko wa pili ambao umechezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Azam FC wakiwa wametoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Simba, Uwanja wa Azam Complex wameibuka na ushindi huo ugenini.

Mabao yote mawili yamepachikwa na nyota Ayoub Lyanga ambaye alitupia dk ya 20 na 54 hivyo kwenye kila kipindi nyota huyo alikuwa anatupia bao.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar ni Said Ndemla ndiye ambaye alipachika bao pekee la kufutia machozi ilikuwa dk ya 80.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad