BEKI wa Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho msimu wa 2021/22 ametua ndani ya kikosi cha Singida Big Stars.
Yanga jana Julai 2 iliweza kukamilisha msimu kwa kutwaa Kombe la Shirikisho kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Coastal Union kwa ushindi wa penalti 4-1 baada ya dk 120 kukamilika kwa kufungana mabao 3-3,Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Taarifa kutoka Singida Big Stars imeweka wazi kuwa:"Tumefanikiwa kuinasa saini ya beki no 2 kutoka kwa mabingwa wa kihistoria nchini Tanzania Yanga. Godfrey amesaini mkataba wa miaka 2 kuitumikia timu yetu,".

No comments:
Post a Comment