PABLO:MCHEZO WETU DHIDI YA AZAM FC UTAKUWA NA UPINZANI MKUBWA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 31 December 2021

PABLO:MCHEZO WETU DHIDI YA AZAM FC UTAKUWA NA UPINZANI MKUBWA

 


PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa Azam FC ni moja ya timu imara na ina wachezaji wazuri hivyo kuelekea kwenye mchezo wao wa kesho Januari Mosi 2022 wanatarajia kupata upinzani mkubwa.

Aidha Pablo amebainisha kwamba ambacho wanahitaji kwenye mchezo huo ni ushindi kwa kuwa maandalizi yameanza kwa muda mrefu na wachezaji wanatambua kwamba wanapaswa kufanya kazi kubwa katika kutoa burudani na kutimiza majukumu yao.

"Nina amini kwamba utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia kwamba Azam FC wana timu nzuri nimewaona kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Ruvu Shooting namna ambavyo walicheza pamoja na mechi nyingine.

"Kikubwa ambacho kitatokea uwanjani ni burudani na wachezaji wanajua kwamba tunahitaji ushinda. Haitakuwa kazi rahisi lakini tutapambana kufanya vizuri na mashabiki wajitokeze kuweza kupata burudani," amesema Pablo. 

Mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zimetoka kushinda mechi zao za mwisho kwa idadi sawa ya mabao ambapo Simba ilishinda mabao 4-1 dhidi ya KMC na Azam FC ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Ruvu Shooting.

Wachezaji wa Simba wanaendelea na mazoezi na miongoni mwa hao ni pamoja na Henock Inonga, Pascal Wawa, Jonas Mkude na Mzamiru Yassin.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad