Post Top Ad
Saturday, 9 August 2025
Friday, 11 July 2025
BEKI MPYA SINGIDA BLACK STARS AFUNGUKA
NYOTA Kelvin Kijili ambaye ni ingizo jipya ndani ya Singida Black Stars akitokea kikosi cha Simba SC ameweka wazi kuwa yupo tayari kwa ajili ya kupambana kutimiza majukumu kwenye timu hiyo kitaifa na kimataifa.
Kijili ametambulishwa rasmi ndani ya Singida Black Stars Julai 10 2025 ikiwa ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya Singida Black Stars.
Msimu wa 2024/25 alikuwa ndani ya kikosi cha Simba SC. Kwenye kikosi cha Simba SC hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza hakufikisha mechi 15 za ligi kati ya 30 ambazo timu hiyo ilicheza.
Anajiunga na Singida Black Stars ambayo itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye aliwahi kuifundisha Yanga SC.
Kijili amesema: "Nimefurahi kusaini mkataba ndani ya Singida Black Stars nina amini kwamba nitafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu kitaifa na kimataifa."
Ni miaka miwili amesaini mchezaji huyo kwa ajili ya changamoto mpya msimu wa 2025/26 amerejea nyumbani kwa mara nyingine tena.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.
CLATOUS CHAMA KWENYE RADA ZA ZESCO UNITED
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga SC, Clatous Chama anatajwa kuwa kwenye rada za Klabu ya Zesco United ya Zambia.
Chama ambaye alitambulishwa rasmi Yanga SC Julai Mosi 2024, mkataba wake wa mwaka mmoja umeggota mwisho.
Alitambulishwa hapo akiwa mchezaji huru akitokea kikosi cha Simba SC ambacho kimegotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Taarifa zinaeleza kuwa mazungumzo ya wakala wa Chama na Zesco United yamefikia kwenye hatua nzuri kilichobaki nyota huyo kusaini na kutambulishwa ikiwa mabosi wa Yanga SC watamchunia moja kwa moja.
Yanga SC wanatambua mkataba wa mchezaji huyo umeisha na hawajafanya mazungumzo yoyote jambo linaloashiria kwamba ni asilimia kubwa hatakuwa kwenye ligi namba nne kwa ubora Afrika Clatous Chama msimu wa 2025/26.
Msimu wa 2024/25, Chama alifunga mabao sita na katika mabao hayo mabao mawili alifunga kwa mapigo huru akiwa nje ya 18.
Imeandikwa
na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo,
kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya
Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa
Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa
Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo
Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.
Sunday, 20 April 2025
FOUNTAIN GATE WAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA
WAPINZANI wa Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara kuelekea kwenye mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa Aprili 21 2025 Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa Fountain Gate wamebainisha kuwa wamepata mbinu za wapinzani wao hivyo wanajua namna watakavyofanya kazi kuwadhibiti.
Yanga ni vinara ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya mechi 25 ni pointi 67 wamekusanya kibindoni na safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 64 ikiwa ni safu kali kwenye kumalizia nafasi ambazo zinatengenezwa ndani ya uwanja kwenye ligi.
Inakutana na Fountain Gate ambayo namba mbili kwa timu ambazo zimeruhusu mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 47 baada yakucheza mechi 26 ikiwa nafasi ya 9 na pointi zake kibindoni ni 29.
Issa Mbuzi amesema kuwa wanatambua ubora wa Yanga ulipo na udhaifu kwa kuwa waliwatazama kwa ukaribu kwenye mchezo dhidi ya Stand United uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex, Aprili 15 2025 na ubao ukasoma Yanga 8-1 Stand United.
“Tunawatambua vizuri hawa Yanga na kwenye mchezo wao dhidi ya Stand tulikuwa na wataalamu wakusoma mbinu zaidi ya wanne, wameniambia wameona namna itakayotupa matokeo kwenye mchezo wetu Aprili 21 tukiwa nyumbani.
“Eneo la kiungo kuna matatizo pale na wanaye Aziz Ki ambaye huyu tutampa mtu wakutembea naye hatua kwa hatua ndani ya uwanja, utakuwa mchezo mgumu lakini tunahitaji pointi tatu zao ili tujihakikishie nafasi ya sita kwenye msimamo.”
Imeandikwa na
Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata
TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika,
usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa
Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa
unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja
Damu usipange kukosa.
Sunday, 2 June 2024
SIMBA KUJIPANGA UPYA TENA
UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utafanyia kazi makosa ambayo yamepita ili kurejea kwenye ubora wao kwa kuwa nyakati ambazo wamepita zimewaumiza.
Ipo wazi kuwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda imegotea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 69.
Kwenye mchezo wa funga msimu 2023/24 ilikuwa ni dhidi ya Geita Gold waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 watupiaji wakiwa ni Saido Ntibanzokiza na Willy Onana.
Imepishana
na taji la ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika na inakwenda kushuhudia
bingwa mpya wa CRDB Federation Cup akipatikana leo kati ya Azam FC na Yanga,
fainali inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Ahmed Ally,
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa nyakati ambazo
wamepitia ni ngumu na hazijawafurahisha hivyo wanapambana kurejea kwenye ubora.
“Hatujapenda na tumekuwa na huzuni kwa kuwa tumepoteza kila kitu ambacho tulikuwa
tunakipigania kwenye msimu ulioisha.
“Yote kwa
yote yaliyopita tunayachukua na tunakwenda kuyafanyia kazi kwa ajili ya kuwa
bora wakati ujao mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”
Tuesday, 2 April 2024
JESHI LA YANGA LITAKALOIBUKA KWA MADIBA HILI HAPA
MSAFARA wa kikosi cha Yanga umekwea pipa mapema Aprili 2 2024 kuwafuata wapinzani wao Mamelodi Sundowns kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa unaotarajiwa kuchezwa Aprili 5 siku ya Ijumaa.
Ni mchezo wa hatua ya robo fainali ikiwa ni mkondo wa pili baada ya ule uliochezwa Machi 30 ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 0-0 Mamelodi Sundowns.
Hiki hapa kikosi cha Yanga chenye wachezaji 26 namna hii:-
Djigui
Diarra, Aboutwalib Mshery na Metacha
Mnata kwa upande wa makipa ambapo chaguo la kwanza ni Diarra
Bakari
Mwamnyeto, Ibrahim
Bacca, Dickson
Job, Yao
Attohoula, Nickson
Kibabage, Joyce
Lomalisa, Gift
Fred na Kibwana
Shomari upande wa mabeki.
Viungo wa ukabaji ni Khalid
Aucho, Zawadi
Mauya, Salum
Abubakar, (Sure Boy), Jonas
Mkude, Mudathir Yahya na Maxi
Nzengeli
Viungo washambuliaji kuna Pacome Zouzoua, Aziz Ki, Augustine Okrah, Skudu Makudubela, Farid
Mussa
na Denis
Nkane.
Washambuliaji ni Clement
Mzize, Joseph
Guede na Kennedy
Musonda ambapo kwenye mchezo wa Uwanja wa Mkapa wote walipata nafasi ya kuchez.
Wednesday, 27 March 2024
MNYAMA AMVUTIA KASI MWARABU KWA MKAPA KIMATAIFA
KIKOSI cha Simba kimerejea Dar baada ya kuweka kambi Zanzibar kwa muda ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Ni Machi 29 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa
ambapo kwa sasa hamasa zinaendelea mtaa kwa mtaa kuwahamasisha mashabiki wa
Simba kujitokeza Uwanja wa Mkapa kushuhudia mchezo huo.
Ahmed Ally, Meneje wa Idara ya Habari na
Mawasiliano Simba amesema kuwa Ijumaa kazi ni moja kwa mashabiki kujitokeza
uwanjani kushangilia mwanzo mwisho katika mchezo huo na malengo ni kuona
wanapata ushindi ndani ya dakika 90.
KOCHA APEWA MAJUKUMU MAZITO
Ally amesema kuwa uzoefu alionao kocha wa
timu hiyo ni moja ya sababu itakayoongeza nguvu kwa timu hiyo kuvuka hatua ya
robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na kutinga hatua ya nusu fainali.
Ikumbukwe kwamba Simba hesabu kubwa kwa msimu
huu ni kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kugotea mara kwa mara hatua ya
robo fainali jambo ambalo limewafanya viongozi wa timu hiyo kubainisha kwamba
inatosha.
"Kwa uzoefu na ubora wa kocha Abdelhak
Benchikha tunaamini atatuvuzusha kwenda Nusu Fainali.
Tunaamini kwamba kila kitu kinawezekana na hilo
linatupa nguvu kwa ajili ya kuwa kwenye ushindani mkubwa ambao upo ndani ya
uwanja kwa kuwa kila kitu kinawezekana na muda ni sasa.
“Hakuna
katika dunia hii mtu yoyote wakuwazuia mashabiki wa Simba wanapotaka jambo lao,
tuungane tupige goti tufanye kila linalowezekana ili tutimize malengo yetu.
“Wachezaji ni wasikivu na wanatambua kazi kubwa
inahitajika kufanyika uwanjani hivyo muda ni sasa kuwa kwenye mpango kazi wa
kutafuta ushindi ndani ya uwanja, mashabiki tujitokeze kwa wingi kwani kila
mchezaji anapenda kuona furaha inabaki ndani ya Simba.
ULINZI KUONGEZEWA DOZI
Benchi la ufundi la Simba limebainisha kuwa
makosa ambayo yamekuwa yakifanyika kwenye mechi za ligi yanafanyiwa kazi kwa
umakini ili kuwa na safu imara ya ulinzi kwenye mechi zao wanazocheza kutokana
na ushindani kuwa mkubwa kitaifa na kimataifa.
Kwenye safu ya ulinzi ni Henock Inonga, Che
Malone, Mohmaed Hussein, Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji wanaounda
safu ya ulinzi ya timu hiyo ya Simba ambayo ina kazi kupambana dhidi ya Al
Ahly.
Ipo wazi kwamba ndani ya Ligi Kuu Bara, safu
ya ulinzi ya Simba haijawa kwenye mwendo bora katika mechi zake tofauti na zile
inazocheza kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba
amesema kuwa wanatambua makosa yalipo jambo linalowafanya wafanye kazi kwa
umakini kuelekea kwenye mechi zijazo kwa kuwaongezea wachezaji wao dozi
nyingine.
“Unaona kwenye mechi ambazo tunacheza
tunapata ushindi na wakati mwingine tunawapa ruhusa wapinzani kutufunga huwa
tunaongea na wachezaji na tutaongeza dozi nyingine kwenye uwanja wa mazoezi.
“Kikubwa ni kuwa makini kwa kuwa mchezo wa
mpira ni mchezo wa makosa, kuelekea kwenye mechi zetu zijazo tuna imani
tutakuwa imara hilo linawezekana kutokana na wachezaji kujituma na kutimiza
majukumu yao kwa ushirikiano,”.
Kikosi cha Simba baada ya kucheza mechi 19
ndani ya ligi ni mabao 18 ukuta umeruhusu ikiwa namba moja kwa timu ambazo
zimefungwa mabao mengi ndani ya tatu bora msimu wa 2023/24.
AL AHLY NDANI YA DAR
Kete inayofuata kwa Simba ni Machi 30 2024
itakuwa dhidi ya Al Ahly ambao tayari Machi 27 wameanza mapema safari kwa ajili
ya kuwasili Dar kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.
Mchezo ujao kwa Simba ni wa Ligi ya Mabingwa
Afrika itakuwa dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 29
tayari wapinzani wao wameanza safari kuja Dar wanatarajiwa kuwasili Machi 27
kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea katika mchezo huo.
Kila timu inautazama mchezo huo kwa hesabu
kubwa za kupata ushindi kutokana na ukubwa wa mashindano hayo barani Afrika.
Tuesday, 19 March 2024
FEISAL SALUM ANA BALAA HUYO
KIUNGO wa Azam FC Feisal Salum ni namba moja kwa nyota wenye mabao mengi ndani ya kikosi cha Azam FC akiwa kafikisha mabao 13.
Nyota huyo yupo sawa na kiungo mshambuliaji wa Yanga Aziz KI ambaye naye katupia jumla ya mabao 13
msimu wa 2023/24 ikiwa kila mmoja yupo kwenye ubora wake katika kutimiza
majukumu yake.
Safu ya Azam
FC kwenye upande wa ushambuliaji ni namba mbili ndani ya timu ambazo zipo tatu
bora ikiwa imefunga jumla ya mabao 47 baada ya kucheza jumla ya mechi 21.
Mbali na
kuwa na mabao 47 pia timu hiyo imekusanya pointi 47 kwenye msimamo ikiwa namba
mbili msimu wa 2023/24 ambao ushindani ni mkubwa tofauti yake na vinara wa ligi
ambao ni Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ni pointi tano pekee.
Wakati Azam
FC ikiwa nafasi ya pili na mabao yake 47 Yanga wao wapo nafasi ya kwanza wakiwa
wamecheza jumla ya mechi 20 pekee kete 10 zimebaki kukamilisha mzunguko wa
pili.
Thursday, 14 March 2024
HESABU ZA YANGA KWA GEITA GOLD ZIPO NAMNA HII
MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo wa leo dhidi ya Geita Gold na wanahitaji kupata pointi tatu wakiwa katika mpango mkubwa wa kupata pointi tatu kwenye mchezo ambao wanaamini utakuwa na ushindani mkubwa.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 2:15 usiku ikiwa ni mzunguko wa pili,ikumbukwe kwamba mzunguko wa kwanza Yanga ilikomba pointi tatu.
Gamondi amesema:"Tumejiandaa vizuri kucheza na Geita Gold, tunafahamu kila mpinzani kuna namna yake ya kujiandaa kimbinu, Ukitazama matokeo yao ya hivi karibuni wameimarika hivyo lazima tuchukue tahadhari ya kutosha bila kujali matokeo yetu ya awali.
“Nina wachezaji wengi wazuri sana, tunaweza kucheza aina yoyote ya mchezo, iwe kushambulia, kumiliki mpira nk. Tunaweza kubadilika badilika kulingana na matakwa ya mchezo kabla na wakati wa mchezo, sijawahi kucheza na aina moja ya falsafa huwa nabadilika kulingana na namna mpinzani anavyocheza na namna navyoweza kumkabili.
“Mechi tatu tumefunga magoli 15, tumeruhusu mabao 3, kimsingi hizi ni takwimu bora siwezi kusema kwamba Geita nao tutawafunga magoli mengi huo utakuwa ubashiri sifanyi kazi ya kubashiri.
"Ninachoweza kufanya kwa sasa ni kujiandaa kushinda mchezo. Tumejiandaa kucheza nao kwa namna yoyote ambayo watajipanga, nafikiri watakuja na mbinu za kujilinda lakini hainipi hofu kwa sababu nina vijana wazuri,".
Thursday, 7 March 2024
FEI TOTO ANA BALAA ZITO UWANJANI
KIUNGO wa matajiri wa Dar, Azam FC Feisal Salum amekuwa kwenye ubora wake katika mechi za hivi karibuni ndani ya Ligi Kuu Bara akifanya kazi kubwa kwenye kutimiza majukumu yake.
Yote haya
yanatokana na ushindani uliopo uwanjani huku Fei Toto akikamilisha kazi yake
kwa umakini na kuwapa furaha mashabiki wa Azam FC wanaoifuatilia timu hiyo
inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwenye mechi za ushindani.
Nyota huyo
anayevaa jezi namba 6 mgongoni ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Yusuph Dabo raia
wa Senegel ambaye ameweka wazi kuwa kila mchezaji ndani ya kikosi hicho ana
nafasi ya kufanya vizuri na makosa ambayo yamekuwa yanatokeo uwanjani
wanayafanyia kazi eneo la mazoezi.
Azam FC
imekuwa na mwendo mzuri kwenye mzunguko wa pili kwa kupata pointi kwenye mechi
zote walizocheza Uwanja wa Azam Complex na safu ya ushambuliaji ikifunga mabao
matano kwenye mechi mbili walizocheza wakiwa nyumbani.
Dabo
amesema: “Kazi kubwa inafanyika kwa kila mchezaji kutimiza majukumu yake na ipo
hivyo kila wakati jambo ambalo linaongeza nguvu kwenye kutimiza majukumu yetu
na kupata ushindi ndani ya uwanja.
“Wakati
mwingine tumekuwa tukishinwa kupata matokeo jambo ambalo linatokea hivyo
kikubwa ni kuona tunakuwa kwenye mwendelezo mzuri kwa kuwa kinachohitajika ni ushindi
na tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa.
“Sio Feisal
pekee bali kila mchezaji anatimiza majukumu yake hili ni jambo la msingi, pale
ambapo tunashindwa kupata matokeo makosa tunafanyia kazi eneo la mazoezi ili
kuwa bora kwa mechi zinazofuata,”.
Fei Toto
kwenye mechi mbili zilizochezwa Uwanja wa Azam Complex alifunga jumla ya mabao
matatu. Ubora wa Fei Toto ulichangia kupatikana kwa pointi nne kati ya pointi
sita ambazo zilikuwa zinasakwa uwanjani ndani ya dakika 90.
Nyota huyo
alifunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa Uwanja wa
Azam Complex ambao baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 4-1 Azam FC
walipokomba pointi tatu jumlajumla.
Mchezo wa
pili kufunga bao ilikuwa dhidi ya Coastal Union uliochezwa hapohapo Azam
Complex ilikuwa ni Machi 6 ubao wa uliposoma Azam FC 1-1 Coastal Union wababe
hao wakagawana pointi mojamoja.
Kwenye
mchezo dhidi ya Coastal Union alifunga bao lililowapa pointi moja dakika za
jioni kwa kuwa Azam FC walikuwa nyuma kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani
mkubwa dhidi ya Wagosi wa Kaya kutoka Tanga.
Fei alifunga
bao hilo dakika ya 81 akiweka usawa bao ambalo lilifungwa na Semfuko Charlse
dakika ya 68. Jumla anafikisha mabao 12 kwenye ligi akiwa ni kinara wa utupiaji
mabao.
Mechi 20
Azam imecheza kwenye ligi ikiwa nafasi ya kwanza kibindoni imekusanya pointi 44
na safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 45 msimu wa 2023/24.
Ikumbukwe
kwamba licha ya kuwa ni kinara wa mabao akiwa nayo 12 kwenye ligi Fei ni mfungaji
wa bao la kwanza ndani ya Azam FC kwenye ligi ilikuwa dhidi ya Tabora United
mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Katika
mchezo huo bao la Fei Toto la ufunguzi lilifungwa dakika ya 3 ikiwa ni mwanzo
wa msimu wa 2023/24 na rekodi nyingine aliyonayo ni mfungaji wa kwanza hat
trick ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 alipofunga kwenye mchezo dhidi ya
Tabora United.
Kazi kubwa
ni kwenye mwendelezo wa kusaka pointi tatu ndani ya ligi huku kiungo huyo
akiweka wazi kwamba kila mchezo kwao wanauchukulia kwa umuhimu ili kupata ushindi.
“Kila mchezo
tunashirikiana na wachezaji wote ili kupata pointi tatu muhimu pale ambapo
tunakosa huwa tunarejea kwenye uwanja wa mazoezi kufanyia kazi makosa yetu hiyo
huwa inakuwa kazi ya benchi la ufundi kwenye kufanya maboresho yetu.
“Ushindani
ni mkubwa na bado tunaendelea kushindana ili kupata matokeo, mashabiki wazidi
kuwa pamoja nasi kwa kuwa kila wakati wapo nasi bega kwa bega katika hilo
tunawaomba waendelee kuwa nasi,”
Monday, 4 March 2024
YANGA NA SIMBA ZAWEKA REKODI/ CHAMA PACOME GUMZO
SIMBA na Yanga zimetinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika rekodi kubwa na ya kujivunia kwa Tanzania kwenye ulimwengu wa mpira.
PACOME NI MVURUGAJI KINOMANOMA
MWAMBA Pacome Zouzoa kiungo wa Yanga aliwavuruga Waarabu wa Algeria CR Belouizdad kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Mkapa kutokana na kasi yake na pasi za uhakika akitumia zaidi mguu wake wa kulia.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 4-0 CR Belouizdad katika mchezo wa hatua ya makundi ikitinga hatua ya robo fainali na mchezo wake wa kufungia kazi kwenye makundi ilipoteza dhidi ya Al Ahly 1-0 Yanga.
Mabao kwenye mchezo dhidi ya Waarabu wa Algeria yalifungwa na Mudathir Yahya, Kennedy Musonda, Aziz KI na Joseph Guede ambaye bao lake la dakika ya 84 liliwapa uhakika Yanga kutinga hatua ya robo fainali.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Februari 24 Pacome kwa kususika kwenye miguso zaidi ya 60 ambapo alitumia mguu wa kulia kutoa jumla ya pasi 37, pasi tatu kwa mguu wa kushoto, alikokota mpira mara 15 na alipiga mashuti yaliyolenga lango mawili miguso kwa kichwa ilikuwa mara mbili alitoa pasi moja ya bao kwenye mchezo huo.
Katika pasi alizotoa kwa mguu wa kulia ni nne pekee hazikuwafikia walengwa aliokuwa akiwapa ndani ya uwanja alipokomba jumla ya dakika 90 kwenye mchezo huo.
Ukiweka kando Pacome mwenye mabao matatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, kipa Djigui Diarra langoni aliokoa hatari saba ilikuwa dakika ya 4, 16, 45, 60,66, 85 na 88.
Pacome amesema kuwa ni furaha kwa timu kiujumla kwa malengo yao kupata ushindi pamoja na mashabiki kupata furaha waliyokuwa wakiifikiria kwa muda mrefu.
“Tulikuwa tunahitaji ushindi na tumepata kwa kilichotokea kwetu ni furaha, tunawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wetu ambao ulikuwa ni muhimu kupata ushindi,”.
Saturday, 2 March 2024
Wednesday, 28 February 2024
SIMBA VITANI KWA MARA NYINGINE TENA
WAKIWA kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ambao utaamua hatma ya Simba kugotea hatua ya makundi ama hatua ya robo fainali leo wana vita nyingine kusaka ushindi mchezo wa raundi ya tatu Kombe la Azam Sports Federation.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku mshindi atasonga mbele kumenyana na Mashujaa ambao walipita raundi ya tatu.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Ahmed Ally ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo utakuwa na ushindani mkubwa lakini maandalizi yao yapo sawa na wanatambua wana vita nyingine Jumamosi.
"Kabla ya kuvaana na Jwaneng tutakuwa na mchezo dhidi ya wakusanya mapato TRA huu ni mchezo muhimu kwetu tunatambua utakuwa na ushindani mkubwa hatujawafuatilia sana wapinzani wetu lakini tunahitaji ushindi kwenye mchezo huo.
Pia leo Februari 28 Simba wameanza kampeni za hamasa kwa ajili ya kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Kuhusu hilo Ally amesema: "Jumamosi tunakwenda kuingia robo fainali kwa mara ya tano mfululizo, kwetu sisi kuingia robo ni jambo la kawaida. Tumezoea kucheza robo na hatujawahi kuishia makundi tangu tumeanza kampeni yetu ya kimataifa.
“Tulimuua AS Vita wa moto, tulimuua USGN, tulimuua Horoya hatuwezi kushindwa kwa Jwaneng Galaxy. Simba anapoitaka robo fainali hakuna wa kutuzuia hata timu zingine zote duniani zitengeneze timu moja. Jwaneng amekuja wakati mbaya, muda ambao tunataka kulipiza kisasi.
“Lilitukaa rohoni lakini muda wa kumtemea nyongo Jwaneng Galaxy, tulikaa na maumivu kwa miaka mitatu na la pili tunataka kuingia robo fainali. Hatuwezi kufungwa na timu inayoburuza mkia katika kundi letu. Tutafanya kila kinachowezekana ilimradi Simba ipate ushindi siku hiyo na hakuna kinachoshindikana. Iwe ardhini, angani au chini ya bahari.
“Tunawaahidi na kuwahakikishia Wanasimba kama kuna kitu kinahitajika hata kiwe kinapatikana chini ya bahari tutakifanya ili Simba iende robo fainali. Jumamosi ni kwenda kumalizia kazi. Hatuwezi kushindwa kwenda robo fainali, yani waporipori wamefuzu alafu sisi wenye mashindano tushindwe? Jumamosi saa 1 usiku tunakutana kumaliza kazi," amesema.
Monday, 26 February 2024
SIMBA YATUMA UJUMBE HUU KIMATAIFA
UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo wao wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy Uwanja wa Mkapa wanachohitaji ni ushindi.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa mshindi anakata tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali ambapo tayari Yanga imeshakata tiketi hiyo baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya CR Belouizdad mabao 4-0 Uwanja wa Mkapa.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuongeza nguvu ya timu hiyo kutinga hatua ya robo fainali.
“Mechi dhidi ya Jwaneng Galaxy itachezwa Jumamosi Machi 2, 2024 saa 1:00 usiku. Licha ya mapendekezo yetu kucheza mechi saa 10:00 jioni lakini CAF wameamua iwe saa 1:00 usiku ili michezo yote iwe muda mmoja.
“Kikosi kimerejea nchini na leo jioni tutaanza rasmi mazoezi kujiandaa na mchezo Jwaneng Galaxy na mchezo wa ASFC dhidi TRA ambao tutacheza Jumatano kwenye uwanja wa Azam Complex.
“Waamuzi wa mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy wataanza kuwasili nchini kuanzia tarehe 29 mwezi huu na wote wanatokea nchini Ghana.
“Mpaka sasa hatujapata taarifa rasmi Jwaneng Galaxy lini watawasili nchini lakini watu wao wa maandalizi ya awali wameshawasili nchini.
“Ushindi wa aina yoyote ambao tutapata Jumamosi sisi tutafuzu bila kujali Wydad kapata ushindi wa aina gani. Sisi na Wydad tukishinda tutakuwa na alama tisa na kanuni ya kwanza ya CAF inaangalia Head to Head, mechi ya kwanza walitufunga goli 1-0 na sisi tukawafunga 2-0.
“Tukifanikiwa kufuzu robo fainali tutakuwa tumeungana na timu zingine kubwa barani Afrika ambazo zimewahi kuingia robo fainali mara nne mfululizo. Hapa nazungumzia Al Ahly, Mamelodi, Wydad na TP Mazembe na sisi tunakwenda kuwa timu ya tano.”
“Tangu tumeanza kampeni ya kimataifa hatujawahi kuishia hatua ya makundi, hatujawahi kufungwa mechi ya mwisho ya maamuzi ya kwenda robo fainali. Simba Sports Club inapofika hatua kama hii anakuwa mnyama mwingine wa ajabu.
“Hatujawahi na hatutakuja kuishia hatua ya makundi, achana na watu wanaochanganyikiwa na ushindi wa goli 4, Mnyama tumeshamfanya mtu goli 7 na tukaenda robo fainali," amesema Ally.
Sunday, 25 February 2024
ALI KAMWE ISHU YAKE IPO HIVI
UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa Ali Kamwe kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupata changamoto za kiafya ghafla usiku wa Februari 24 2024.
Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ushindi unaowapeleka moja kwa moja hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Muda mchache kabla ya mchezo huo kugota mwisho, Kamwe alipata changamoto hiyo na kukimbizwa hospitali mapema kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
Taarifa ambayo imetolewa na Yanga imeweka wazi kuwa kiongozi huyo ambaye anaingia kwenye rekodi ya mashuhuda wa Yanga kutinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika anaendelea vizuri.
"Wananchi, Ofisa habari wetu Ali Kamwe alipata changamoto dakika chache kabla ya mchezo wetu kuisha na kukimbizwa hospitali ya Aga Khan kupata matibabu. Hivi sasa anaendelea vizuri na yuko salama salmin.,".
Thursday, 22 February 2024
SIMBA KAMILI GADO KUWAKABILI ASEC MIMOSAS
Mikael Igendia Meneja wa Simba amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
Ijumaa Simba inakibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapaubao ulisoma Simba 1-1 ASEC Mimosas hivyo waligawaa pointi mojamoja ndani ya kundi B.
Vinara ni ASEC wakiwa na pointi 10 huku Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi tano kibindoni baada ya kucheza mechi 4.
Meneja huyo amesema: "Ni mchezo mgumu ambao tunakwenda kucheza, mazingira yanatupa ruhusa kufanya vizuri kwa kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kutafuta ushindi.
"Kikubwa ni kusubiri muda wa mchezo kwani wachezaji waliopo wapo tayari licha ya wengine kukosekana kutokana na sababu mbalimbali lakini tupo tayari.
"Tutamkosa Ayoub Lakred kutokana na kadi za njano, John Bocco na Willy Onana hawa walipata maumivu lakini wanaendelea vizuri,".
Baadhi ya wachezaji ambao wapo Ivory Coast ni pamoja na Henock Inonga, Clatous Chama, Mzamiru Yassin, Kibu Dennis.
ALVES MIAKA MINNE AHUKUMIWA
MAHAKAMA ya juu ya Catalonia nchini Hispania imemuhukumu kutumikia jela miaka minne na nusu nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil na Klabu ya Barcelona Dani Alves .
Alves mwenye miaka 40 amehukumiwa adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kosa la shambulio la ngono au unyanyasaji wa kingono kwa Mwanamke mmoja kwenye Club ya usiku.
Alves ambaye amekua rumande tangu 2023 akisubiri hukumu hii, ametakiwa kumlipa fidia ya euro 150,000 (Tsh milioni 414) Mwanamke huyo.
Ipo wazi kuwa Dani Alves ni mchezaji namba mbili mwenye makombe mengi zaidi duniani sasa anakwenda kupokonywa uhuru wake kwa miaka 4.
Hatojiamulia chochote kuanzia sasa, maisha yake yatakuwa chini ya ulinzi wa mwingine. Kwa miaka minne taka yake itabaki kuwa takataka.
Taka ya wenye mamlaka ndio taka. Ukiitazama sura yake, hauoni ule ukatili wake akiwa uwanjani anapambana na mawinga bora kabisa.
Kizimba kimeondoka na ule ujasiri wake wa kuweka mwili wake popote kuzuia bao ndani ya uwanja.
Uso wake umesawajika, labda anajutia kilichopelekea yote haya? Hatujui. Labda anaamini ameonewa kwa kilichotokea? Hatufahamu.
Tunachojua, kesi inayompeleka jela ni unyanyasaji wa kijinsia. Iwe ni kweli ama la, bado huu ni muendelezo wa anguko la mwanaume nyuma ya kinyago kilekile alichokizoea.
Hadithi iliyoanza kwa mwanamke kutenda dhambi ya kula tunda akiwa kwenye bustani ya Mungu.
Na mwisho mwanaume kupewa adhabu ya kuteseka duniani.
Pole Dani Alves ameandika Kasese Aziz.
Wednesday, 21 February 2024
GAMONDI AWAPA TANO WACHEZAJI ISHU YA 5G
MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema wachezaji wamejituma na kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja mbele ya Polisi Tanzania.
Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa watetezi wa Kombe la Azam Sports Federation walipata ushindi kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Februari 20 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 5-0 Polisi Tanzania na mabao yakifungwa na Joseph Guede aliyefunga mabao mawili dakika ya 13 na 45 huku Farid Mussa dakika ya 33 akipachika bao moja, Clement Mzize alipachika bao moja dakika ya 82 na kamba ya tano ni mali ya Shekhan Khamis dakika ya 86 kwa penalti.
Nyota Guede na Okra kwenye mchezo huo walifanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wachezaji wengine kufunga na kutoa pasi za mabao ambayo kazi hiyo ilifanywa na Okra.
Gamond amesema: "Wachezaji wamejituma kwenye kutimiza majukumu yao katika hilo tunapawa pongezi na tunaamini kwamba kazi bado inaendelea kwa ajili ya mechi zijazo,'.
Tuesday, 20 February 2024
ONANA/ AYOUB LAKRED/ CHASAMBI OUT SIMBA
KIKOSI cha Simba chenye jumla ya nyota 22 kimekwea pipa kuelekea Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas unaotarajiwa kuchezwa Februari 23 nchini Ivory Coast.
Ipo wazi kwamba huo ni mchezo wa pili hatua ya makundi ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 1-1 ASEC Mimosas bao la Simba lilifungwa na Saido Ntibanzokiza kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na Kibu Dennis.
Kwenye msafara wa Simba umewajumuisha makipa watatu ambao ni Aishi Manula,Ally Salim na Hussein Abel. Upande wa ulinzi ni Shomari Kapombe, Israel Mwenda, David Kameta, (Duchu), Mohamed Hussein, Henock Inonga, Che Malone, Kennedy Juma, Hussen Kazi.
Eneo la viungo kuna Babacarr Sarr, Sadio Kanoute, Fabrince Ngoma, Mzamiru Yassin, Abdallah Khamis, Saido Ntibanzokiza,Kibu Dennis, Kibu Dennis, Luis Miquissone, Clatous Chama na upande wa washambuliaji ni Pa Omary Jobe na Fredy Michael.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa mpango mkubwa ni kutafuta ushindi kwenye mchezo hhuo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kila timu kutafuta matokeo.
Ipo wazi kwamba kipa Ayoub Lakred atakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kadi za njano huku kiungo mshambuliaji Willy Onana yeye bado hajawa fiti.
Wengine ambao hawapo kwenye kikosi hicho ni Ladack Chasambi, John Bocco ambaye ni nahodha, Saleh Karabaka, Kramo, Edwin Balua.
"Tunakwenda Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa ambao ni muhimu kwetu kupata ushindi hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kuelekea kwenye mchezo wetu. Wapo wachezaji ambao watakosekana kutokana na sababu mbalimbali kutoka kwenye benchi la ufundi,".
Duchu ameweka wazi kwamba wanatambua utakuwa mchezo mgumu lakini wanakwenda kuwakilisha vema bendera ya Tanzania kimataifa.
"Hautakuwa mchezo mwepesi na hatuna kazi nyepesi kikubwa ni kuona kwamba tunapata ushindi kwenye mchezo wetu ambao ni muhimu kupata matokeo,".