UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utafanyia kazi makosa ambayo yamepita ili kurejea kwenye ubora wao kwa kuwa nyakati ambazo wamepita zimewaumiza.
Ipo wazi kuwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda imegotea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 69.
Kwenye mchezo wa funga msimu 2023/24 ilikuwa ni dhidi ya Geita Gold waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 watupiaji wakiwa ni Saido Ntibanzokiza na Willy Onana.
Imepishana
na taji la ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika na inakwenda kushuhudia
bingwa mpya wa CRDB Federation Cup akipatikana leo kati ya Azam FC na Yanga,
fainali inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Ahmed Ally,
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa nyakati ambazo
wamepitia ni ngumu na hazijawafurahisha hivyo wanapambana kurejea kwenye ubora.
“Hatujapenda na tumekuwa na huzuni kwa kuwa tumepoteza kila kitu ambacho tulikuwa
tunakipigania kwenye msimu ulioisha.
“Yote kwa
yote yaliyopita tunayachukua na tunakwenda kuyafanyia kazi kwa ajili ya kuwa
bora wakati ujao mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”
No comments:
Post a Comment