WAWAKILISHI wa Tanzania watakuwa kazini kwenye mechi za kimataifa ikiwa ni katika Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tanzania inawakilishwa na nchi nne ambazo ni Simba SC na Yanga SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Azam FC dhidi ya Singida Black Stars.
Ni Jumamosi, Yanga SC watakuwa Uwanja wa Bingu nchini Malawi wakicheza na Silver Striker, kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na itarushwa mubashara kupitia AzamSports2HD.
Jumapili, Simba SC watakuwa Eswatini katika Uwanja wa Somhlolo wakicheza na Nsingizini Hotspurs kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 10:00 jioni na kuruka mubashara kupitia AzamSports2HD.
Kwa Kombe la Shirikisho Afrika ipo namna hii:-
Jumamosi, KMKM watakuwa nyumbani Uwanja wa Amaan wakiwakaribisha matajiri wa Chamazi, Azam FC.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 10:15 jioni na kuruka mubashara kupitia AzamSports4HD.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 10:15 jioni na kuruka mubashara kupitia AzamSports4HD.
Jumapili, Singida BS watakuwa jijini Bunjumbura katika Uwanja wa Prince Louis Rwagasore wakicheza na Flambeau Du Centre.
Mechi hii itachezwa kuanzia saa 10:00 jioni, na itakuwa mubashara kupitia AzamSports4HD.

No comments:
Post a Comment