KATIBU wa chama cha waigizaji Tanzania mkoani Pwani (TFDAA)
Kadnas Nassoro amesema kuwa ubinafsi ni tatizo kubwa linalosababisha tasnia
isiweze kufanya vema zaidi kwa wasanii wengi wa filamu na muziki nchini.
Akizungumza hivi
karibuni amesema kuwa hali ya kila msanii kujiona yeye ni bora kuliko mwenzake
na kutopenda kushirikiana na wasanii wengine kunawaponza wengi na kuwafanya
washindwe kufanikiwa.
Katibu wa chama cha wasanii mkoani Pwani (TFDAA) Kadnas Nassoro |
“Kila msanii anataka kuonekana yeye ni bora kuliko wenzake
katika tasnia hicho kitu hakitakiwi tunapaswa kushirikiana katika kila namna
ili tuweze kudumisha umoja utakaotuletea mafanikio zaidi”alisema
Naye Mwenyekiti wa TFDAA mkoa wa Pwani Vendavenda Sumuni
amewataka wasanii wajitokeze kwa wingi kujiunga katika umoja huo ili wawe na
sauti moja katika kufuatilia haki zao na kuhakikisha kila msanii
anafikia
malengo.
“Mkiwa na umoja ni sawa na kuwa na sauti moja yenye nguvu
hali itakayofanya tuweze kufanya vizuri katika tasnia yetu na kuweza kusaidia
kuinua vipaji zaidi hivyo nawasihi tuungane katika umoja huu”amesema
Chama hicho kilianzisha mwaka 2011 chini ya Mike Sangu
kikiwa na lengo la kuimarisha umoja wa wasanii kinasimamiwa na diwani wa kata
ya Mtambani Mkoani Pwani wilaya ya Kibaha Godfrey Mwafulilwa .
Kina jumla ya wanachama 100 na kimeweza kusimamia uzalishaji
wa filamu pamoja na tamthilia ya siri ya nafsi pamoja na filamu zilizopo sokoni
ambazo ni pamoja na Bingo,Mzimu wa Nyangiti,who is he,heri ya jana na nyingine
nyingi zinazofanya vizuri sokoni.
Good Work Bro. Improve more and more
ReplyDelete