NYOTA Kelvin Kijili ambaye ni ingizo jipya ndani ya Singida Black Stars akitokea kikosi cha Simba SC ameweka wazi kuwa yupo tayari kwa ajili ya kupambana kutimiza majukumu kwenye timu hiyo kitaifa na kimataifa.Kijili ametambulishwa rasmi ndani ya Singida Black Stars Julai 10 2025 ikiwa ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya Singida Black Stars.
Msimu wa 2024/25 alikuwa ndani ya kikosi cha Simba SC. Kwenye kikosi cha Simba SC hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza hakufikisha mechi 15 za ligi kati ya 30 ambazo timu hiyo ilicheza.
Anajiunga na Singida Black Stars ambayo itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye aliwahi kuifundisha Yanga SC.
Kijili amesema: "Nimefurahi kusaini mkataba ndani ya Singida Black Stars nina amini kwamba nitafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu kitaifa na kimataifa."
Ni miaka miwili amesaini mchezaji huyo kwa ajili ya changamoto mpya msimu wa 2025/26 amerejea nyumbani kwa mara nyingine tena.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.
No comments:
Post a Comment