Dizo Click

Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Post Top Ad

Tuesday 2 April 2024

JESHI LA YANGA LITAKALOIBUKA KWA MADIBA HILI HAPA

11:12 0

 


MSAFARA wa kikosi cha Yanga umekwea pipa mapema Aprili 2 2024 kuwafuata wapinzani wao Mamelodi Sundowns kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa unaotarajiwa kuchezwa Aprili 5 siku ya Ijumaa.

Ni mchezo wa hatua ya robo fainali ikiwa ni mkondo wa pili baada ya ule uliochezwa Machi 30 ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 0-0 Mamelodi Sundowns.

Hiki hapa kikosi cha Yanga chenye wachezaji 26 namna hii:-

Djigui Diarra,
 Aboutwalib Mshery na  Metacha Mnata kwa upande wa makipa ambapo chaguo la kwanza ni Diarra
 Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca,  Dickson Job, Yao Attohoula, Nickson Kibabage, Joyce Lomalisa, Gift Fred na Kibwana Shomari upande wa mabeki.

Viungo wa ukabaji ni  Khalid Aucho, Zawadi Mauya, Salum Abubakar, (Sure Boy), Jonas Mkude, Mudathir Yahya na Maxi Nzengeli

Viungo washambuliaji kuna Pacome Zouzoua, Aziz Ki, Augustine Okrah, Skudu Makudubela, Farid Mussa
na Denis Nkane.


Washambuliaji ni Clement Mzize,  Joseph Guede na Kennedy Musonda ambapo kwenye mchezo wa Uwanja wa Mkapa wote walipata nafasi ya kuchez.

Read More

Wednesday 27 March 2024

MNYAMA AMVUTIA KASI MWARABU KWA MKAPA KIMATAIFA

13:01 0

 


KIKOSI cha Simba kimerejea Dar baada ya kuweka kambi Zanzibar kwa muda ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni Machi 29 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa ambapo kwa sasa hamasa zinaendelea mtaa kwa mtaa kuwahamasisha mashabiki wa Simba kujitokeza Uwanja wa Mkapa kushuhudia mchezo huo.

Ahmed Ally, Meneje wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa Ijumaa kazi ni moja kwa mashabiki kujitokeza uwanjani kushangilia mwanzo mwisho katika mchezo huo na malengo ni kuona wanapata ushindi ndani ya dakika 90.

 

 

KOCHA APEWA MAJUKUMU MAZITO

Ally amesema kuwa uzoefu alionao kocha wa timu hiyo ni moja ya sababu itakayoongeza nguvu kwa timu hiyo kuvuka hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na kutinga hatua ya nusu fainali.

Ikumbukwe kwamba Simba hesabu kubwa kwa msimu huu ni kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kugotea mara kwa mara hatua ya robo fainali jambo ambalo limewafanya viongozi wa timu hiyo kubainisha kwamba inatosha.

"Kwa uzoefu na ubora wa kocha Abdelhak Benchikha tunaamini atatuvuzusha kwenda Nusu Fainali.

Tunaamini kwamba kila kitu kinawezekana na hilo linatupa nguvu kwa ajili ya kuwa kwenye ushindani mkubwa ambao upo ndani ya uwanja kwa kuwa kila kitu kinawezekana na muda ni sasa.

 “Hakuna katika dunia hii mtu yoyote wakuwazuia mashabiki wa Simba wanapotaka jambo lao, tuungane tupige goti tufanye kila linalowezekana ili tutimize malengo yetu.

“Wachezaji ni wasikivu na wanatambua kazi kubwa inahitajika kufanyika uwanjani hivyo muda ni sasa kuwa kwenye mpango kazi wa kutafuta ushindi ndani ya uwanja, mashabiki tujitokeze kwa wingi kwani kila mchezaji anapenda kuona furaha inabaki ndani ya Simba.

ULINZI KUONGEZEWA DOZI

Benchi la ufundi la Simba limebainisha kuwa makosa ambayo yamekuwa yakifanyika kwenye mechi za ligi yanafanyiwa kazi kwa umakini ili kuwa na safu imara ya ulinzi kwenye mechi zao wanazocheza kutokana na ushindani kuwa mkubwa kitaifa na kimataifa.

Kwenye safu ya ulinzi ni Henock Inonga, Che Malone, Mohmaed Hussein, Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji wanaounda safu ya ulinzi ya timu hiyo ya Simba ambayo ina kazi kupambana dhidi ya Al Ahly.

Ipo wazi kwamba ndani ya Ligi Kuu Bara, safu ya ulinzi ya Simba haijawa kwenye mwendo bora katika mechi zake tofauti na zile inazocheza kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wanatambua makosa yalipo jambo linalowafanya wafanye kazi kwa umakini kuelekea kwenye mechi zijazo kwa kuwaongezea wachezaji wao dozi nyingine.

“Unaona kwenye mechi ambazo tunacheza tunapata ushindi na wakati mwingine tunawapa ruhusa wapinzani kutufunga huwa tunaongea na wachezaji na tutaongeza dozi nyingine kwenye uwanja wa mazoezi.

“Kikubwa ni kuwa makini kwa kuwa mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa, kuelekea kwenye mechi zetu zijazo tuna imani tutakuwa imara hilo linawezekana kutokana na wachezaji kujituma na kutimiza majukumu yao kwa ushirikiano,”.

Kikosi cha Simba baada ya kucheza mechi 19 ndani ya ligi ni mabao 18 ukuta umeruhusu ikiwa namba moja kwa timu ambazo zimefungwa mabao mengi ndani ya tatu bora msimu wa 2023/24.

AL AHLY NDANI YA DAR

Kete inayofuata kwa Simba ni Machi 30 2024 itakuwa dhidi ya Al Ahly ambao tayari Machi 27 wameanza mapema safari kwa ajili ya kuwasili Dar kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.

Mchezo ujao kwa Simba ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 29 tayari wapinzani wao wameanza safari kuja Dar wanatarajiwa kuwasili Machi 27 kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea katika mchezo huo.

Kila timu inautazama mchezo huo kwa hesabu kubwa za kupata ushindi kutokana na ukubwa wa mashindano hayo barani Afrika.

 

Read More

Tuesday 19 March 2024

FEISAL SALUM ANA BALAA HUYO

09:33 0


KIUNGO wa Azam FC Feisal  Salum ni namba moja kwa nyota wenye mabao mengi ndani ya kikosi cha Azam FC akiwa kafikisha mabao 13.

Nyota huyo yupo sawa na kiungo mshambuliaji wa Yanga Aziz KI ambaye naye katupia jumla ya mabao 13 msimu wa 2023/24 ikiwa kila mmoja yupo kwenye ubora wake katika kutimiza majukumu yake.

Safu ya Azam FC kwenye upande wa ushambuliaji ni namba mbili ndani ya timu ambazo zipo tatu bora ikiwa imefunga jumla ya mabao 47 baada ya kucheza jumla ya mechi 21.

Mbali na kuwa na mabao 47 pia timu hiyo imekusanya pointi 47 kwenye msimamo ikiwa namba mbili msimu wa 2023/24 ambao ushindani ni mkubwa tofauti yake na vinara wa ligi ambao ni Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ni pointi tano pekee.

Wakati Azam FC ikiwa nafasi ya pili na mabao yake 47 Yanga wao wapo nafasi ya kwanza wakiwa wamecheza jumla ya mechi 20 pekee kete 10 zimebaki kukamilisha mzunguko wa pili.

Read More

Thursday 14 March 2024

HESABU ZA YANGA KWA GEITA GOLD ZIPO NAMNA HII

18:52 0

 


MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo wa leo dhidi ya Geita Gold na wanahitaji kupata pointi tatu wakiwa katika mpango mkubwa wa kupata pointi tatu kwenye mchezo ambao wanaamini utakuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 2:15 usiku ikiwa ni mzunguko wa pili,ikumbukwe kwamba mzunguko wa kwanza Yanga ilikomba pointi tatu.

Gamondi amesema:"Tumejiandaa vizuri kucheza na Geita Gold, tunafahamu kila mpinzani kuna namna yake ya kujiandaa kimbinu, Ukitazama matokeo yao ya hivi karibuni wameimarika hivyo lazima tuchukue tahadhari ya kutosha bila kujali matokeo yetu ya awali.

“Nina wachezaji wengi wazuri sana, tunaweza kucheza aina yoyote ya mchezo, iwe kushambulia, kumiliki mpira nk. Tunaweza kubadilika badilika kulingana na matakwa ya mchezo kabla na wakati wa mchezo, sijawahi kucheza na aina moja ya falsafa huwa nabadilika kulingana na namna mpinzani anavyocheza na namna navyoweza kumkabili.

“Mechi tatu tumefunga magoli 15, tumeruhusu mabao 3, kimsingi hizi ni takwimu bora siwezi kusema kwamba Geita nao tutawafunga magoli mengi huo utakuwa ubashiri sifanyi kazi ya kubashiri.

 "Ninachoweza kufanya kwa sasa ni kujiandaa kushinda mchezo. Tumejiandaa kucheza nao kwa namna yoyote ambayo watajipanga, nafikiri watakuja na mbinu za kujilinda lakini hainipi hofu kwa sababu nina vijana wazuri,".

Read More

Thursday 7 March 2024

FEI TOTO ANA BALAA ZITO UWANJANI

19:23 0

 


KIUNGO wa matajiri wa Dar, Azam FC Feisal Salum amekuwa kwenye ubora wake katika mechi za hivi karibuni ndani ya Ligi Kuu Bara akifanya kazi kubwa kwenye kutimiza majukumu yake.

Yote haya yanatokana na ushindani uliopo uwanjani huku Fei Toto akikamilisha kazi yake kwa umakini na kuwapa furaha mashabiki wa Azam FC wanaoifuatilia timu hiyo inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwenye mechi za ushindani.

Nyota huyo anayevaa jezi namba 6 mgongoni ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Yusuph Dabo raia wa Senegel ambaye ameweka wazi kuwa kila mchezaji ndani ya kikosi hicho ana nafasi ya kufanya vizuri na makosa ambayo yamekuwa yanatokeo uwanjani wanayafanyia kazi eneo la mazoezi.

Azam FC imekuwa na mwendo mzuri kwenye mzunguko wa pili kwa kupata pointi kwenye mechi zote walizocheza Uwanja wa Azam Complex na safu ya ushambuliaji ikifunga mabao matano kwenye mechi mbili walizocheza wakiwa nyumbani.

Dabo amesema: “Kazi kubwa inafanyika kwa kila mchezaji kutimiza majukumu yake na ipo hivyo kila wakati jambo ambalo linaongeza nguvu kwenye kutimiza majukumu yetu na kupata ushindi ndani ya uwanja.

“Wakati mwingine tumekuwa tukishinwa kupata matokeo jambo ambalo linatokea hivyo kikubwa ni kuona tunakuwa kwenye mwendelezo mzuri kwa kuwa kinachohitajika ni ushindi na tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa.

“Sio Feisal pekee bali kila mchezaji anatimiza majukumu yake hili ni jambo la msingi, pale ambapo tunashindwa kupata matokeo makosa tunafanyia kazi eneo la mazoezi ili kuwa bora kwa mechi zinazofuata,”.

Fei Toto kwenye mechi mbili zilizochezwa Uwanja wa Azam Complex alifunga jumla ya mabao matatu. Ubora wa Fei Toto ulichangia kupatikana kwa pointi nne kati ya pointi sita ambazo zilikuwa zinasakwa uwanjani ndani ya dakika 90.

Nyota huyo alifunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ambao baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 4-1 Azam FC walipokomba pointi tatu jumlajumla.

Mchezo wa pili kufunga bao ilikuwa dhidi ya Coastal Union uliochezwa hapohapo Azam Complex ilikuwa ni Machi 6 ubao wa uliposoma Azam FC 1-1 Coastal Union wababe hao wakagawana pointi mojamoja.

Kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union alifunga bao lililowapa pointi moja dakika za jioni kwa kuwa Azam FC walikuwa nyuma kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa dhidi ya Wagosi wa Kaya kutoka Tanga.

Fei alifunga bao hilo dakika ya 81 akiweka usawa bao ambalo lilifungwa na Semfuko Charlse dakika ya 68. Jumla anafikisha mabao 12 kwenye ligi akiwa ni kinara wa utupiaji mabao.

Mechi 20 Azam imecheza kwenye ligi ikiwa nafasi ya kwanza kibindoni imekusanya pointi 44 na safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 45 msimu wa 2023/24.

Ikumbukwe kwamba licha ya kuwa ni kinara wa mabao akiwa nayo 12 kwenye ligi Fei ni mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Azam FC kwenye ligi ilikuwa dhidi ya Tabora United mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Katika mchezo huo bao la Fei Toto la ufunguzi lilifungwa dakika ya 3 ikiwa ni mwanzo wa msimu wa 2023/24 na rekodi nyingine aliyonayo ni mfungaji wa kwanza hat trick ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 alipofunga kwenye mchezo dhidi ya Tabora United.

Kazi kubwa ni kwenye mwendelezo wa kusaka pointi tatu ndani ya ligi huku kiungo huyo akiweka wazi kwamba kila mchezo kwao wanauchukulia kwa umuhimu ili kupata ushindi.

“Kila mchezo tunashirikiana na wachezaji wote ili kupata pointi tatu muhimu pale ambapo tunakosa huwa tunarejea kwenye uwanja wa mazoezi kufanyia kazi makosa yetu hiyo huwa inakuwa kazi ya benchi la ufundi kwenye kufanya maboresho yetu.

“Ushindani ni mkubwa na bado tunaendelea kushindana ili kupata matokeo, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwa kuwa kila wakati wapo nasi bega kwa bega katika hilo tunawaomba waendelee kuwa nasi,”

 

Read More

Monday 4 March 2024

YANGA NA SIMBA ZAWEKA REKODI/ CHAMA PACOME GUMZO

15:14 0

 


SIMBA na Yanga zimetinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika rekodi kubwa na ya kujivunia kwa Tanzania kwenye ulimwengu wa mpira.

Kufika kwao hatua ya nusu fainali ni mipango makini na maandalizi mazuri mmoja kati yao huenda atakutana na Mamelod Sundowns hawa miamba kabisa kutoka Afrika Kusini.
Droo inatarajiwa kuchezwa hivi karibu ambapo Simba haitakutana na ASEC Mimosas kwa kuwa walikuwa kundi moja kama ilivyo Yanga haitakutana na AL Ahly ya Misri.
Gumzo kubwa ni eneo la kiungo kwa timu zote mbili Yanga mwamba Pacome na Simba ni mwamba Chama.

Kila mmoja kwa nyakati zake ametimiza majukumu yake ambapo Pacome anaingia kwenye rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyefunga bao dhidi ya Al Ahly kwenye hatua ya makundi mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Chama kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy alikuwa na siku nzuri kazini alipofunga bao moja na kutoa pasi moja ya mchezo wakati Simba ikifanikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Read More

PACOME NI MVURUGAJI KINOMANOMA

15:00 0

 


MWAMBA Pacome Zouzoa kiungo wa Yanga aliwavuruga Waarabu wa Algeria CR Belouizdad kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Mkapa kutokana na kasi yake na pasi za uhakika akitumia zaidi mguu wake wa kulia.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 4-0 CR Belouizdad katika mchezo wa hatua ya makundi ikitinga hatua ya robo fainali na mchezo wake wa kufungia kazi kwenye makundi ilipoteza dhidi ya Al Ahly 1-0 Yanga.

Mabao kwenye mchezo dhidi ya Waarabu wa Algeria yalifungwa na Mudathir Yahya, Kennedy Musonda, Aziz KI na Joseph Guede ambaye bao lake la dakika ya 84 liliwapa uhakika Yanga kutinga hatua ya robo fainali.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Februari 24 Pacome kwa kususika kwenye miguso zaidi ya 60 ambapo alitumia mguu wa kulia kutoa jumla ya pasi 37, pasi tatu kwa mguu wa kushoto, alikokota mpira mara 15 na alipiga mashuti yaliyolenga lango mawili miguso kwa kichwa ilikuwa mara mbili alitoa pasi moja ya bao kwenye mchezo huo.

Katika pasi alizotoa kwa mguu wa kulia ni nne pekee hazikuwafikia walengwa aliokuwa akiwapa ndani ya uwanja alipokomba jumla ya dakika 90 kwenye mchezo huo.

Ukiweka kando Pacome mwenye mabao matatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, kipa Djigui Diarra langoni aliokoa hatari saba ilikuwa dakika ya 4, 16, 45, 60,66, 85 na 88.

Pacome amesema kuwa ni furaha kwa timu kiujumla kwa malengo yao kupata ushindi pamoja na mashabiki kupata furaha waliyokuwa wakiifikiria kwa muda mrefu.

“Tulikuwa tunahitaji ushindi na tumepata kwa kilichotokea kwetu ni furaha, tunawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wetu ambao ulikuwa ni muhimu kupata ushindi,”.

 

Read More

Post Top Ad