Yanga SC yaachana na Romain Folz mazima - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 18 October 2025

Yanga SC yaachana na Romain Folz mazima


RASMI uongozi wa Yanga SC Oktoba 18,2025 umetoa taarifa ya kuachana na Romain Folz ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Mchezo wa mwisho kukaa benchi ni Oktba 18,2025 ubao wa Uwanja wa Bingu umesoma Silver Strikers 1-0 Yanga SC, CAF Champions League.

Taarifa kutoka Yanga SC imeeleza namna hii:-“Uongozi wa Young African Sports Club unapenda kuutarifu Umma kuwa, umevunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Romain Folz.

“Uongozi wa Young African Sports Club unamshukuru kocha Romain Folz kwa mchango wake ndani ya klabu yetu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yanayofata.

“Katika kipindi hiki kikosi chetu kitakuwa chini ya kocha msaidizi Patrick Mabedi huku mchakato wa kutafuta kocha mkuu ukiendelea,” .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad