Simba SC vs Nsingizini kitaumana - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday, 26 October 2025

Simba SC vs Nsingizini kitaumana

 


Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions, kitaumana kwa Mkapa kwa wababe hawa Oktba 26 kila timu kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa kwanza ugenini Oktoba 19,2025 ilikuwa Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC. Mchezo wa maamuzi utapigwa Uwanja wa Mkapa kwa wababe hawa wawili kusaka timu itakayokwenda hatua ya makundi.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa huo ni mchezo wa kazi na watapambana kupata matokeo mazuri uwanjani.

“Kikosi Jumatano  kinarudi Mo Simba Arena kuanza maandalizi ya mchezo wa Jumapili. Tunayo furaha ya kocha wetu Seleman Matola amemaliza adhabu yake hivyo atakuwepo kwenye benchi Jumapili kuendelea na majukumu yake.

“Kuelekea mchezo huu tumeweka viingilio vya kitajiri. Viingilio ni Tanzanite - Tsh. 250,000, Platinum - Tsh. 150,000, VIP A - Tsh. 30,000, VIP B - Tsh. 20,000, VIP C - Tsh. 10,000 na Mzunguko - Tsh. 5,000.

“Afrika hii timu zenye uhakika wa kucheza makundi mara saba mfululizo ni Al Ahly na Mamelodi na sisi tunaongezeka hapo. Ni mechi ambayo inatuongezea thamani kwenye klabu yetu. Na Mwanasimba asitokee akaidharau hii mechi, tuutizame huu mchezo kama mchezo mpya. Itakuwa haina maana yoyote tuje hapa tufungwe bao moja au mbili au twende matuta hatupo tayari kuona hiyo fedheha. Tuhesabu bado ni bilabila.

“Mpaka sasa sisi tumeshinda mechi moja na bado hatujafuzu. Mechi hii ya kufuzu tunataka kujaza uwanja wa Mkapa, hatutakiwi kuchukulia poa, kwenye mpira hakuna kitu cha kawaida. Twendeni tukaujaze Uwanja wa Benjamini Mkapa. Na sare yetu siku ya Jumapili itakuwa ni jezi nyekundu ya kuscan. Usije na jezi ya zamani tafadhali, kila Mwanasimba aje na jezi mpya ya Jayrutty.

“Wanasimba tunasababu za kuja uwanjani maana mechi iliyopita tuliangalizia mchezo tukiwa Coco Beach, ilituuma. Tunalazimika kwenda uwanjani ili kumkaribisha Meneja Dimitar Pantev akutane na Wanasimba kwa mara ya kwanza, aione Simba Sports Club ipoje. Kwa kifupi Oktoba 26 itakuwa Simba Day ya Pantev maana ile nyingine hakuwepo," Semaji Ahmed Ally.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad