CAF Champions League, Oktoba 25 2025 uongozi wa Yanga SC umeweka wazi kuwa mechi hiyo itakuwa mikononi mwa mashabiki hivyo wajitokeze kwa wakati kuishangilia timu hiyo na kuipeleka hatua ya makundi.
Hiyo imetokana na mashabiki wengi kufunga safari kuelekea
nchini Malawi kuishangilia timu hiyo Oktoba 18, 2025 kwenye mchezo wa kwanza
uliochezwa Uwanja wa Bingu matokeo yaliposoma Silver Strikers 1-0 Yanga SC.
Yanga SC inahitaji ushindi wa angalau goli 2-0 katika mchezo
wa Oktoba 25,2025, Uwanja wa Mkapa huku mashabiki wakiombwa kuwa wastaarabu na
wasifanye vurugu yoyote ile wala kuwasha moto wakiwa uwanjani.
Ali Kamwe Ofisa Habari wa
Yanga SC amesema kuwa wanachama wa Yanga SC waliomba mechi ya Jumamosi kusiwe
na viingilio jambo ambalo limefanyiwa kazi na uongozi kwa umakini mkubwa na
kuamua iwe hivyo.
“Tumepokea maoni mengi
kutoka kwa Wanachama wetu wakiuomba uongozi wa Yanga kuwa mechi ya jumamosi
usiwe na viingilio, tuwaachie wao mchezo huu na tuwape nafasi ya wao kuisapoti
timu yetu na kuivusha kwenda hatua ya makundi.
“Tayari uongozi wetu umekutana na kujadili maoni
haya ya wanachama na kimsingi wamelipokea, wamekubaliana na kulipitisha ombi
hili la Wanachama wetu. Hivyo ombi limekubaliwa na mashabiki wawe makini kwenye
mchezo wetu wasilete vurugu.
“Ikitokea ni shabiki wa
Mtibwa Sugar, Mbeya City ama timu yoyote amekuja usimsumbue muache aangalie
mpira apate burudani lakini akija a malengo tofauti huyo lazima aondolewe kwa
kuonyeshwa mlango wa kutokea,” Ally Kamwe

No comments:
Post a Comment