Simba SC vs Nsingizini Hotspurs , Kibu Dennis kwenye kazi nyingine - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 20 October 2025

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs , Kibu Dennis kwenye kazi nyingine


AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa bado hawajatinga hatua ya makundi kutokana na ugumu wa kila mchezo CAF Champions League.

Simba SC Oktoba 19,2025 ilipata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Nsingizini Hotspurs uliochezwa Uwanja wa Somholo, mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa Oktoba 26,2025 Uwanja wa Mkapa.

“Tumepata ushindi wa mabao 3-0 ugenini haya matokeo ni zawadi kwa mashabiki wa Eswatini, hawa Nsingizni sio timu ya kubeza hata kidogo kazi haijaisha,”.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Somhlolo, nchini Eswatini ulikuwa na ushindani mkubwa. Kipindi cha kwanza timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu, huku Simba SC wakifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi. Bao la kwanza la mchezo huo lilikuja dakika ya 45 ya mchezo, kupitia kwa mlinzio wa Simba SC, Wilson Nangu.

Nangu alifunga bao hilo la kuongoza kwa kuunganisha kwa kichwa krosi nzuri ya kona ya kiungo, Neo Maema. Mara tu, baada ya bao hilo kipyenga cha mwamuzi kikasikika na timu Kwenda mapumziko.

Kibu Dennis ambaye aliingia kipindi cha pili alifunga maao mawili dakika ya 82 na 89 amebainisha kuwa bado wana kazi nyingine kuelekea mchezo wa marudiano Uwanja wa Mkapa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad