NAIBU Murugenzi masuala ya wateja wa huduma na
bidhaa za mawasiliano (TCRA) Thadayo Ringo amewataka wananchi kuhakikisha kuwa wanasoma masharti ya mitandao kabla ya kujiunga na endapo kutakuwa na makosa sheria itafuata mkondo wake .
![]() |
| Naibu Mkurugenzi masuala ya wateja wa huduma na bidhaa za mawasiliano (tcra) Thadayo Ringo akifafanua kuhusu matumizi ya mitandao |
Akizungumza na mwandishi wa habari hii katika jukwaa la sanaa lililofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) alisema kuwa matatizo mengine yanaweza kutatuliwa kutokana na
makubaliano wakati wa kujiunga
“Hakuna huduma inayotolewa bila ya kuwa na masharti hivyo
kuna ulazima wa kila mmoja anayejiunga kuhakikisha kuwa anasoma vizuri masharti
na kuhakikisha anaelewa kwa undani vigezo vilivyowekwa ili aweze kujiunga na
huduma hiyo”alisema.
Aidha alisema kuwa mamlaka ya mawasiliano nchini ipo makini
katika kuhakikisha usalama wa taarifa za wateja zinalindwa , kinachowavutia
watu kutumia simu ni uwepo wa utunzaji wa siri za wateja wake hivyo hakuna haja
ya watumiaji kuhofia.
“Ukiwa na mashaka wasiliana na TCRA ili uweze kupata
ufafanuzi pia hakikisha kabla hujapost
kitu unauhakika nacho kwani hauwezi kufuta kumbukumbu iliyo kwenye mtandao ukishatuma
Onesmo Kayanda Mkurugenzi wa fedha na utawala BASATA alisema
kuwa kuna umuhimu wa kuwa makini kwa kila taarifa ambayo inatumwa na mteja ili
kuhakikisha usalama wake kwani kufanya jambo ambalo litakuwa kinyume hatua
lazima zichukuliwe.

This comment has been removed by the author.
ReplyDelete