Sekta ya utalii kuongeza pato la taifa - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 5 July 2017

Sekta ya utalii kuongeza pato la taifa



NAIBU katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Aloyce Nzuki  amesema kuwa Serikali  ina mpango wa kuinua kipato cha nchi kupitia sekta ya utalii ambayo ina fursa nyingi zinazoweza kuinua uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa.

Uzinduzi wa ripoti ya umoja wa mataifa inayohusu maendeleo ya uchumi ya UNCTAD  ambayo imeangazia sekta ya utalii na uchumi  Kuanzia kushoto ni Prosper Charle,Onesmo Keneth na Naibu Katibu Mkuu wizara ya maliasili na  Utalii Aloyce Nzuki
Akizungumza Da r es salaam katika ukumbi wa mikutano wa shirika la kazi  Duniani(ILO) kwenye uzinduzi wa ripoti ya maendeleo ya kiuchumi ya UNCTAD 2017 ambayo imeangazia sekta ya utalii na uchumi alisema kuwa utalii ni miongoni mwa raslimali ambayo inauwezo wa kuongeza
mapato kupitia kodi.

“Tuna  sehemu nyingi zenye vivutio hali ambayo inaweza kuongeza mapato kwani  sehemu kubwa inayotumika kwa sasa  kufanyia utalii kuwa ni kanda za kaskazini pekee hivyo tuna mradi wa kuongeza sehemu za kanda ya Magharibi pamoja na Kusini”.

Alisema kuwa wamegundua sehemu nyingine ambayo ni kivutio zaidi kwa watalii kama fukwe za bahari ambazo zipo kandokando ya bahari ya hindi maeneo ya Dar es Salaam pamoja na Tanga ambayo hayatumiki katika shughuli za utalii hivyo wapo kwenye mkakati kuyachukua.

Prosper Charle ambaye ni mchumi katika masuala ya maendeleo alisema kuwa Tanzania ipo kwenye kufanya mageuzi ya uchumi katika sekta ya viwanda hivyo kuna haja ya kupanua wigo wa mapato ambapo utalii pia ni miongoni mwa sekta inayoweza kuleta maendeleo.


“Endapo kutakuwa na maboresho hasa kwenye miundombinu  itakuwa ni kivutio kikubwa kwa watalii kuweza kufika maeneo bila wasiwasi hali  itakayoongeza idadi ya watalii kuweza kufika kwenye maeneo yenye vivutio pamoja na kuwekeza kwenye utalii wa ndani”alisema 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad