RAIS wa shirikisho la filamu Tanzania(TAFF) Simon Mwakifamba
amewataka wasanii kuokwenye kazingeza
juhudi kwa kuongeza ujuzi wa kutengeneza
filamu pamoja na kubadilisha aina za wahusika wakuu wanaowatumia kuchezaza
filamu.
![]() |
| Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba |
Akizungumza na wasanii wa filamu na wadau wa sanaa katika ukumbi wa Baraza la
Sanaaa Taifa alisema mapito wanayopitia
wasanii yatakwisha ni ya muda kutokana
na kile ambacho kimepandwa na wasanii wenyewe hali inayofanya wavune maumivu
kwa kushindwa kutengeneza kazi zenye utofauti.
“Watazamaji wamekuwa na ujuzi mkubwa kuliko watengeneza
filamu hali inayosababisha kazi kudorora sokoni hivyo ili kuweza kulishinda
jambo hili kuna ulazima wa kuwa wabunifu kwa kujifunza bila kuchoka ili waweze
kutengeneza kitu cha kipekee”alisema Mwakifamba.
Alisema kuwa kukua kwa sanaa kunategemea na dhamira ya
msanii mwenyewe kwa kile anachokiamini ndiko kunaweza kuleta mabadiliko sio kuishia kulalamika kuwa hakuna mauzo
ilihali wasanii wenyewe ni wachangiaji .
“Ili kufikia mabadiliko lazima tujiandae kwenye fikra sio
kuwa na mawazo finyu ambayo sio chachu ya kuelekea kule tunakohitaji lazima
tukubali kuwa tumekosea tujipange upya kuboresha yale ambayo ni mapungufu
yetu”alisema
Alisema kuwa kutokubali kuibua vipaji vipya kunaiponza
tasnia ya filamu kwani waigizaji wenye majina wamekuwa wakirudia kucheza filamu
hali inayofanya kushindwa kutofautisha
aina ya filamu kwa kuwa hakuna kitu cha kuwatofautisha katika kazi mpya.

No comments:
Post a Comment