Mkondo: Msikate tamaa - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday, 29 June 2017

Mkondo: Msikate tamaa


MHARIRI mkuu wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo Bakari Mkondo amewataka wanafunzi kujituma kwa juhudi  katika masomo na kazi ili waweze kufikia malengo yao katika tasnia ya uandishi wa habari

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam wakifundishwa namna ya kubuni kurasa na msanifu wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo Kulthumu Matanda
Akizungumza na wanafunzi wa chuo cha uadishi wa habari Dar es Salaam (DSJ)  waliofanya ziara ya masomo ofisini hapo alisema kuwa fani ya uandishi inamtaka mwanafunzi kujitoa na kuhakikisha
thisisdizo444@gmail,comkuwa anatumia muda mwingi kufikiria kufanya vizuri .

“Kujifunza ni siku zote hivyo kuna haja ya kuhakikisha kuwa mazoezi yanafanywa kwa vitendo hasa kwa kuandika habari  ambazo zinafuata misingi ya uandishi wa habari ambazo  zinazingatia kanuni hazina dalili ya udanganyifu katika tasnia ya uandishi”alisema Mkondo.

Mhariri wa habari Stephen Baligeya aliwataka wanafunzi kuzingatia miiko ya uandishi wa habari ili kuweza kuepuka kesi zisizo za lazima katika uandishi jambo ambalo sio jema kwa mwandishi aliyekaa darasani.

“Umakini wa kuzingatia maadili hasa katika uandishi ni kitu cha msingi kwani hakuna kazi isiyozingatia maadili haiwezi kupata nafasi ya kumtambulisha mwandishi katika tasnia zaidi ya kushusha hadhi yake ya taaluma”alisema


Ana Andrew ambaye ni balozi wa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam alisema kuwa ziara imemuongezea ujuzi hasa kwa kuweza kujifunza namna ya mpangilio wa gazeti unavyokuwa na mbinu za uandishi wa habari ambazo zitakuwamwongozo katik kazi yake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad