Waandishi waaswa kuwa wabunifu - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday, 29 June 2017

Waandishi waaswa kuwa wabunifu


MBUNIFU wa gazeti la Uhuru na mzalendo Kuruthum Matanda amewataka wanafunzi  wa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ) kutumia ujuzi wao katika utendaji wa kazi ili waweze kuwa tofauti na wengine katika tasnia ya uandishi wa habari.
Mbunifu kurasa Kuruthumu Matanda kushoto akiwaelekeza namna kazi inavyofanyika wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ) walipotembelea ofisi za Uhuru na Mzalendo

Akizungumza na wanafnzi hao waliotembelea  ofisi ya Uhuru katika ziara ya masomo alisema kuwa kujifunza ni jambo lisilokuwa na kikomo kwa watu wote.

“Hakuna kitu kigumu hivyo ujuzi ambao unao ni mtaji tosha katika kuhakikisha kuwa unafanikisha ndoto zako kwani hakuna kinachoshindikana endapo utaamua kwa moyo wa dhati kufanya hi lo jambo”alisema

Athanas Kazige ambaye ni mhariri wa Michezo gazeti la Uhuru na Mzalendo alisema kuwa wanafunzi wasizahau kanuni wanazofundishwa kuhusu uandishi pamoja na kuongeza mbinu za kikomando katika kuhakikisha wanapata ukweli.

“Mengi yanatokea hasa katika kutafuta habari jambo la kuzingatia ni kuhakikisha unatumia mbinu kamili ambazo zitakupa nafasi ya kupata kile unachohitaji ili uweze kuujuza umma kinachoendelea kwani kazi kubwa ya mwandishi ni kuhakikisha anatoa taarifa za kweli”alisema Kazige.


Baraka Michel mwanafunzi wa ngazi ya cheti kwa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam alisema kuwa ziara za masomo zinawajenga katika kuhakikisha kuwa wanatambua namna ya kutafuta habari mpaka kukamilika kuripotiwa kwa jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad