Usalama wa watoto bado unalegalega - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 27 June 2017

Usalama wa watoto bado unalegalega


LICHA ya jitihada kubwa ambazo zinafanywa na Jeshi la polisi katika kuhakikisha kuwa ulinzi na usalama wa raia unaimirika hasa kipindi cha sikukuu bado wananchi wamelitupia lawama jeshi hilo kwa kupuuzia usalama wa watoto.

Bado si salama maeneo ya kuogea watoto kwa kutokuepo kwa vifaa kama maboya ambayo endapo kutatokea na tatizo
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hii maeneo ya Kigamboni , Feri wamesema kuwa kuna haja ya kuimarisha ulinzi hasa kwa  watoto ambao  wengi hupenda kuongelea na kucheza kandokando ya bahari.

“Watotowengi wanapenda kucheza kwenye maji  hivyo kuna umuhimu wa kuongeza usalama hasa kwa kuweka maboya ambayo yatakua msaada kwa wazazi kuwasaidia watoto ama kuwepo na jeshi la majini likifanya doria ”alisema Mohamed.

Ashura Ramadhani ambaye ni Mzazi alisema kuwa yupo karibu na mwanaye ambaye anapenda kuogelea japo anacheza kwenye maji ya kina kifupi bado anahofia endapo ataenda kwenye kina kirefu kwani yeye mwenyewe hajui kuogelea.

“Sina uwezo wa kuogelea mwanangu analilia kucheza kwenye maji hali inayonilazimu nami pia niwe karibu naye hapa hivyo kuna haja ya maeneo kama haya kuwekwa maboya ambayo yatakuwa msaada endapo litatokea tatizo”alisema Ashura .

Kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lucas Mkondya alisema kuwa Jeshi limejipanga vyema kuhakikisha wananchi wanasherehekea  sikukuu kwa amani bila bugudha za ya aina yoyote.


“Uzoefu unaonesha kuwa mara nyingi kipindi cha sikukuu watu wenye nia ovu hujiandaa kufanya vitendo vya kiarifu kutakuwa na doria ya masaa 24 maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu na tutatumia taarifa za kiintelijinsia kuimarisha ulinzi”alisema Mkondya

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad