Usisahau hata wewe ulikuwa mtoto - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 23 June 2017

Usisahau hata wewe ulikuwa mtoto

UWEZO wao mkubwa upo katika kufurahi na kusahau mabaya kwa urahisi hali inayowafanya wajihisi wapo salama hata sehemu yenye hatari kubwa ndio maana hata wakimwona mdudu kama nyoka wanacheka na kumfuata bila hofu.
Uwezo wa kuunda magari ya kuchezea umefanywa na watoto hawa waliopo kituo cha kulea watoto Maunga Kinondoni

Tupo nao kwenye jamii yetu kila siku kila saa wanahitaji uangalizi mkubwa ili wazidi kuwa salama kwani tusipowajali hawa tunapoteza nasi furaha kwa kutumia muda mwingi kuitafuta furaha ambayo
ilikuwa inachezewa nasi wenyewe bila kujua.

Hakuna anayetambua thamani ya kile alichonacho mkononi ndio maana wahenga kwa kulijua hilo
walisema “Mbuzi hakuona thamani ya mkia wake mpaka pale ulipoungua”ni fursa yetu kuwatunza hawa wadogo ambao ndio taifa la kesho.

Mwimbaji makini na mwandika mashairi Judithi Mbibo wengi wanamtambua kama Lady Jay dee aliandika mashairi akisema kuwa Mtoto ni malaika hivyo kuna umuhimu wa kuwatazama  kwa umakini watoto kila wakati na si kipindi cha sikukuu tu.


“Nikichoka kutembea nabebwa,kulala muda niloamua ni vitu ambavyo anavifanya mtoto kutokana na hali ya kupewa mamlaka ya kile anachokitaka japo hana uwezo huo jukumu letu kubwa kuwatunza na kuhakikisha wanatimiza ndoto zao”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad