Dar es Salaam
KATIBU wa soko la Kisutu Suitbert Nyawalle amewataka wazazi wenye tabia ya
kuwaajiri watoto waache kwani kwa
kufanya hivyo kunamfanya awaze sana fedha hali inayodumaza uwezo wa kufikiria
masomo .
| Mtoto akiwa katika biashara ya Karanga |
Akizungumza na mwandishi wa habari hii alisema kuwa mtoto mwenye
umri chini ya 18 bado
anahitaji elimu na matunzo bora ili aweze kujijengea
uwezo wa kufikiri pamoja na kutambua matumizi sahihi ya muda.
“Ukomavu wa akili katika suala la fedha unahitajika hasa kwa
mtoto anatakiwa apewe muda mwingi kujifunza sio kuwa katika ajira isiyo rasmi hivyo kuna
umuhimu wa mzazi kutambua hilo na kumpa fursa ya kuendelea na masomo”alisema
Aidha alisema kuwa hakuna mfanyabiashara anayeruhusiwa
kumwajiri mtoto katika soko hilo ikibainika anapewa adhabu kwani atakuwa
anakiuka mipango ya uongozi pamoja na mkakati wa serikali katika kutokomeza
ajira kwa watoto.
“Adhabu kali kwa anayekiuka agizo la uongozi inahusika kwani
sheria ni msumeno inakata kote kote tuna jukumu la kuwalinda watoto na kuwapa
elimu ili waweze kutusaidia baadaye na sio kuwafanya watutumikie kabla ya
wakati”alisisitiza
No comments:
Post a Comment