MLIMBWENDE wa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam
anayeshikilia taji la Miss DSJ 2016 – 2017 Anna Andrew amewataka wanajamii kuwa
na utamaduni wa kuwatembelea wenye uhitaji .
Akizungumza na mwandishi wa habari hii alisema kuwa karibu
nao kunawafanya waweze kutambua thamani yao kwa kujiona hawana tofauti na wengine ambao wanaishi kwenye mazingira bora.
![]() |
| Ana Andrew Miss DSJ |
Stanley Ackson ambaye ni balozi wa Nishike Mkono alisema
kuwa imefika wakati wa kuonesha upendo
kwa vitendo hasa kwa ndugu zetu ambao wanaishi katika mazingira hatarishi hali
itakayoweza kuwainua wale waliokata tamaa.
“Maneno matupu hayawezi kutosha kwa kuwa kila mmoja ni
bingwa wa kuongea kinachotakiwa ni utekelezaji na kuhakikisha kuwa matendo ndio
yanapewa nafasi katika kila jambo kwani undugu kufaana kama ambavyo wahenga
walisema “alisisitiza Ackson

No comments:
Post a Comment