Kutunza yatima ni agizo la Mungu-Mpinda - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 21 June 2017

Kutunza yatima ni agizo la Mungu-Mpinda

KATIBU wa Maunga Center ambacho ni kituo cha kulea watoto yatima  Rashid Mpinda amewataka wana jamii kuwajali watoto  walio katika mazingira magumu kwani hilo ni agizo la Mungu kwa wote wenye dini na wasiokuwa na dini.

Michezo huimarisha afya ya watoto kama ambavyo walikutwa watoto wa kituo cha kulea yatima cha Maunga Center kilichopo Kinondoni wakicheza kiboleni
Akizungumza na mwandishi wa habari hii alisema kuwa jukumu la kuwatunza yatima ni letu sote na kwa kufanya hivyo tutakuwa tukitimiza maagizo ambayo tuliachiwa na Mwenyezi Mungu hali
itakayotupa  thawabu.

“Wajibu wa kuwatunza watoto ni wetu sote  kuna ulazima wa kuungana pasipokubaguana kwa kuwa sisi sote ni ndugu na wale walio katika mazingira magumu si kwa mapenzi yao kwani hakuna anayependa kuishi maisha magumu”alisema Mpinda.

Aidha alisema kuwa serikali inapaswa kuvithamini vituo vya watoto kwani uhitaji ni mkubwa siku zote wanakwama kuendelea kuwachukua watoto wengine kutokana na uhaba wa eneo hali inayosababisha washindwe kutoa msaada.


“Uhitaji wa eneo kwa ajili ya makazi ya watoto unatufanya tushindwe kuwasaidia watoto wengine hivyo tunapenda kuiomba serikali iweze kutupatia eneo ambalo litatuwezesha kujenga kituo kikubwa zaidi na kutoa matunzo kwa waliokosa nafasi”alisema Mpinda

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad