MSANII wa muziki wa mduara Ally Ramadhani anayetambulika kwa
jina la AT amewataka wasanii kujitoa kwa ajili ya wenye uhitaji ili kuweza kupata
thawabu kwa Mungu kwa kuokoa maisha ya
wanaoishi mazingira magumu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema kila mmoja anapaswa kutambua kwamba kujitoa kwa ajili ya wengine ni jambo la kheri
hakuna wa kuachiwa mzigo hasa linapokuja
suala la kusaidia jamii.
| Watoto wanaolelewa katika kituo cha Maunga Center kilichopo Kinondoni wakiwa katika michezo kukuza uwezo wa akili |
“Kila mmoja anawajibu wa kutambua umuhimu wa kuwasaidia wale
walio katika mazingira magumu kukwepa
majukumu na kuiachia serikali ama kikundi cha aina fulani hilo si jambo jema
kwani wote tupo katika jamii”alisema AT.
Aidha alisema kuwa kujitoa hakuangalii umaarufu ama cheo cha
mtu kila mtu ana wajibu tabia za
vizingizio kwa wasanii wakubwa zisipewe nafasi jambo linalotakiwa ni kuungana
katika kila hali.
“Kwa mwenye kujali na kutambua umuhimu wa umaarufu wake
anawajali wengine pia tunapaswa
kuunganisha nguvu zetu katika kuwasaidia wenzetu kwa kuwashika mkono na
kuwafariji pia hata muda nao ni zawadi
tosha kwao”alisisitiza
No comments:
Post a Comment