Sheria ya mtandao haimuachi mtu salama - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 12 July 2017

Sheria ya mtandao haimuachi mtu salama


 NAIBU Murugenzi  masuala ya wateja wa huduma na bidhaa za mawasiliano (TCRA) Thadayo Ringo amewataka wananchi kuhakikisha kuwa wanasoma masharti ya mitandao kabla ya kujiunga na endapo kutakuwa na makosa sheria itafuata mkondo wake .

Naibu Mkurugenzi masuala ya wateja wa huduma na bidhaa za mawasiliano (tcra) Thadayo Ringo akifafanua kuhusu matumizi ya mitandao 
Akizungumza na mwandishi wa habari hii katika jukwaa la sanaa lililofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) alisema  kuwa matatizo mengine yanaweza kutatuliwa kutokana na
makubaliano wakati wa kujiunga

“Hakuna huduma inayotolewa bila ya kuwa na masharti hivyo kuna ulazima wa kila mmoja anayejiunga kuhakikisha kuwa anasoma vizuri masharti na kuhakikisha anaelewa kwa undani vigezo vilivyowekwa ili aweze kujiunga na huduma hiyo”alisema.

Aidha alisema kuwa mamlaka ya mawasiliano nchini ipo makini katika kuhakikisha usalama wa taarifa za wateja zinalindwa , kinachowavutia watu kutumia simu ni uwepo wa utunzaji wa siri za wateja wake hivyo hakuna haja ya watumiaji kuhofia.

“Ukiwa na mashaka wasiliana na TCRA ili uweze kupata ufafanuzi  pia hakikisha kabla hujapost kitu unauhakika nacho kwani hauwezi kufuta kumbukumbu iliyo kwenye mtandao ukishatuma
 tayari imeshatambulika duniani kote”alisema

Onesmo Kayanda Mkurugenzi wa fedha na utawala BASATA alisema kuwa kuna umuhimu wa kuwa makini kwa kila taarifa ambayo inatumwa na mteja ili kuhakikisha usalama wake kwani kufanya jambo ambalo litakuwa kinyume hatua lazima zichukuliwe.



1 comment:

Post Top Ad