Mitandao ya kijamii Moto chini - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 4 August 2017

Mitandao ya kijamii Moto chini

Na .Victor Denis
Dar es Salaam
JAMII imetakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa kujitangaza hasa ili kuweza kufanya vema katika ushindani wa kibiashara hali itakayoweza kuwapa mafanikio  katika kazi zao..

Akizungumza na wanafunzi wa chuo cha  uandishi wa habari Dar es Salaam wakala wa Google Tanzania Angel Ernest alisema kuwa hakuna kinachoshindikana katika ulimwengu
wa teknolojia ya habari.

“Kuna maana kubwa sana katika matumizi ya kuwa makini katika mitandao ya kijamii uwezo wa wale ambao wanaweza kugharamia masuala kazi za kwenye mitandao wana nafasi ya kufanya vizuri hasa kwenye ushindani na kujipatia kipato “alisema

Aidha aliwataka wanafunzi kuweza kuwa na tabia ya kuwa wepesi katika kuhakikisha kuwa wanatuma habari ambazo zinaishi tofauti na kuishia kutuma picha za kawaida ambazo hazina manaufaa kwa mtu yeyote zaidi ya kujifurahisha tu “ alisema


Zainab Mbaraka ambaye ni Katibu Mkuu Serikali ya Wanafunzi DASJOSO alisema kuwa wamenufaika na semina hiyo kwani imeweza kuwapa mwanga katika hali ya kuwa katika uwezo mpya hasa kwa matumizi ya mitandao ya kijamii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad