MWALIMU wa somo la radio wa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ) Stella Msaliboko amewataka wanafunzi kujituma na kuongeza juhudi katika masomo ya vitendo ili kuongeza ujuzi.
Akizungumza na mwandishi wa Mtaasisi blog amesema kuwa kila mwanafunzi ana wajibu wa kujituma na kufanya mazoezi kwa vitendo zaidi kwa kuwa ujuzi siku siku ni hazina isiyoharibika
"Kila mmoja inampasa kutambua kwamba mazoezi ya vitendo yanakufanya uwe bora na ujue namna ya kuweza kuongeza ujuzi na kutambua makosa yako hivyo ni budi kila mwanafunzi akajituma kufanya mazoezi".Amesema Msaliboko
Salama Athumani ambaye ni waziri wa elimu DSJ amesema kuwa elimu ya vitendo inamjenga mwanafunzi kuwa katika nafasi nzuri ya kutambua kipaji chake na namna gani atarekebisha makosa yake.
"Kujifunza kwa vitendo ni jambo la kheri kwa kuwa linamkuza mwanafunzi katika mazingira ya kutambua ni namna gani ataweza kuondoa
makosa yake kabla hajaingia rasmi kwenye suala la ajira".Amesema
Fatuma Makowa mwanafunzi wa ngazi ya cheti (DSJ) amesema kuwa anaamini kujifunza kwa vitendo kunamkuza mwanafunzi katika ubora wa masomo ya nje na ndani kwa wakati mmoja.
"Mwanafunzi akishiriki masomo kwa vitendo anapata faida mara mbili zaidi kwa kuwa kile anachojifunza darasani ndicho anachokifanyia kazi hivyo anaongeza ujuzi na uelewa pia".Amesema Makowa.
Smita Ratani mwanafunzi wa ngazi ya stashahada DSJ amesema kuwa wanafunzi wanaongeza zaidi maarifa muda wanaofanya vitendo kwa kuwa fani ya uandishi ni utendaji tu unaohitajika kwa juhudi.
"Fani ya uandishi wa habari inahitaji zaidi vitendo kuliko kuacha kwa kupuuzia bila kufanya mazoezi hivyo ni busara kushiriki mazoezi ya vitendo ili kuongeza ujuzi".Amesema Ratani
Akizungumza na mwandishi wa Mtaasisi blog amesema kuwa kila mwanafunzi ana wajibu wa kujituma na kufanya mazoezi kwa vitendo zaidi kwa kuwa ujuzi siku siku ni hazina isiyoharibika
Mwalimu Stella Msaliboko wa DSJ |
Salama Athumani ambaye ni waziri wa elimu DSJ amesema kuwa elimu ya vitendo inamjenga mwanafunzi kuwa katika nafasi nzuri ya kutambua kipaji chake na namna gani atarekebisha makosa yake.
"Kujifunza kwa vitendo ni jambo la kheri kwa kuwa linamkuza mwanafunzi katika mazingira ya kutambua ni namna gani ataweza kuondoa
makosa yake kabla hajaingia rasmi kwenye suala la ajira".Amesema
Fatuma Makowa mwanafunzi wa ngazi ya cheti (DSJ) amesema kuwa anaamini kujifunza kwa vitendo kunamkuza mwanafunzi katika ubora wa masomo ya nje na ndani kwa wakati mmoja.
"Mwanafunzi akishiriki masomo kwa vitendo anapata faida mara mbili zaidi kwa kuwa kile anachojifunza darasani ndicho anachokifanyia kazi hivyo anaongeza ujuzi na uelewa pia".Amesema Makowa.
Smita Ratani mwanafunzi wa ngazi ya stashahada DSJ amesema kuwa wanafunzi wanaongeza zaidi maarifa muda wanaofanya vitendo kwa kuwa fani ya uandishi ni utendaji tu unaohitajika kwa juhudi.
"Fani ya uandishi wa habari inahitaji zaidi vitendo kuliko kuacha kwa kupuuzia bila kufanya mazoezi hivyo ni busara kushiriki mazoezi ya vitendo ili kuongeza ujuzi".Amesema Ratani
No comments:
Post a Comment