ONANA/ AYOUB LAKRED/ CHASAMBI OUT SIMBA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday 20 February 2024

ONANA/ AYOUB LAKRED/ CHASAMBI OUT SIMBA


KIKOSI cha Simba chenye jumla ya nyota 22 kimekwea pipa kuelekea Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas unaotarajiwa kuchezwa Februari 23 nchini Ivory Coast.

Ipo wazi kwamba huo ni mchezo wa pili  hatua ya makundi ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 1-1 ASEC Mimosas bao la Simba lilifungwa na Saido Ntibanzokiza kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na Kibu Dennis.

Kwenye msafara wa Simba umewajumuisha makipa watatu ambao ni Aishi Manula,Ally Salim na Hussein Abel. Upande wa ulinzi ni Shomari Kapombe, Israel Mwenda, David Kameta, (Duchu), Mohamed Hussein, Henock Inonga, Che Malone, Kennedy Juma, Hussen Kazi.

Eneo la viungo kuna Babacarr Sarr, Sadio Kanoute, Fabrince Ngoma, Mzamiru Yassin, Abdallah Khamis, Saido Ntibanzokiza,Kibu Dennis, Kibu Dennis, Luis Miquissone, Clatous Chama na upande wa washambuliaji ni Pa Omary Jobe na Fredy Michael.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa mpango mkubwa ni kutafuta ushindi kwenye mchezo hhuo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kila timu kutafuta matokeo.

Ipo wazi kwamba kipa Ayoub Lakred atakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kadi za njano huku kiungo mshambuliaji Willy Onana yeye bado hajawa fiti.

Wengine ambao hawapo kwenye kikosi hicho ni Ladack Chasambi, John Bocco ambaye ni nahodha, Saleh Karabaka, Kramo, Edwin Balua.


"Tunakwenda Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa ambao ni muhimu kwetu kupata ushindi hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kuelekea kwenye mchezo wetu. Wapo wachezaji ambao watakosekana kutokana na sababu mbalimbali kutoka kwenye benchi la ufundi,".


Duchu ameweka wazi kwamba wanatambua utakuwa mchezo mgumu lakini wanakwenda kuwakilisha vema bendera ya Tanzania kimataifa.

"Hautakuwa mchezo mwepesi na hatuna kazi nyepesi kikubwa ni kuona kwamba tunapata ushindi kwenye mchezo wetu ambao ni muhimu kupata matokeo,".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad