YANGA HESABU NDEFU KIMATAIFA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday 19 February 2024

YANGA HESABU NDEFU KIMATAIFA


KATIKA anga la kimataifa wakiwa na pointi tano kundi D wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga wameweka wazi kuwa malengo yao ni kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo ujao kwa Yanga katika anga la kimataifa ikiwa hatua ya makundi ni dhidi ya CR Belouzidad unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Timu zote mbili zina pointi tano kibindoni hivyo mshindi ataongeza nafasi ya kufikia malengo ya kutinga hata ya robo fainali.

Ali Kamwe Ofisa Habari wa Yanga amesema:" Kundi la kiume ambalo tupo na  nafasi bado iko wazi kwa kila timu. Sisi Yanga fainali yetu ni Uwanja wa Mkapa Vs Belouzidad.

"Mchezo huo utakuwa ni 24/2/2024. Mpango wetu ni robo fainali. Na tutautimiza mpango huu kama tutaungana pamoja na kwenda Uwanjani kuwapa nguvu wachezaji wetu siku hiyo.

"Uwanja kujaa ndio silaha yetu ya kwanza ya kumpunguza makali Mwarabu, mashabiki tujitokeze kwa wingi muda ni sasa,".

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad