SIMBA VITANI KWA MARA NYINGINE TENA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday 28 February 2024

SIMBA VITANI KWA MARA NYINGINE TENA

 


WAKIWA kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ambao utaamua hatma ya Simba kugotea hatua ya makundi ama hatua ya robo fainali leo wana vita nyingine kusaka ushindi mchezo wa raundi ya tatu Kombe la Azam Sports Federation.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku mshindi atasonga mbele kumenyana na Mashujaa ambao walipita raundi ya tatu.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Ahmed Ally ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo utakuwa na ushindani mkubwa lakini maandalizi yao yapo sawa na wanatambua wana vita nyingine Jumamosi.

"Kabla ya kuvaana na Jwaneng tutakuwa na mchezo dhidi ya wakusanya mapato TRA huu ni mchezo muhimu kwetu tunatambua utakuwa na ushindani mkubwa hatujawafuatilia sana wapinzani wetu lakini tunahitaji ushindi kwenye mchezo huo.

Pia leo Februari 28 Simba wameanza kampeni za hamasa kwa ajili ya kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Kuhusu hilo Ally amesema: "Jumamosi tunakwenda kuingia robo fainali kwa mara ya tano mfululizo, kwetu sisi kuingia robo ni jambo la kawaida. Tumezoea kucheza robo na hatujawahi kuishia makundi tangu tumeanza kampeni yetu ya kimataifa.

“Tulimuua AS Vita wa moto, tulimuua USGN, tulimuua Horoya hatuwezi kushindwa kwa Jwaneng Galaxy. Simba anapoitaka robo fainali hakuna wa kutuzuia hata timu zingine zote duniani zitengeneze timu moja. Jwaneng amekuja wakati mbaya, muda ambao tunataka kulipiza kisasi.

“Lilitukaa rohoni lakini muda wa kumtemea nyongo Jwaneng Galaxy, tulikaa na maumivu kwa miaka mitatu na la pili tunataka kuingia robo fainali. Hatuwezi kufungwa na timu inayoburuza mkia katika kundi letu. Tutafanya kila kinachowezekana ilimradi Simba ipate ushindi siku hiyo na hakuna kinachoshindikana. Iwe ardhini, angani au chini ya bahari.

“Tunawaahidi na kuwahakikishia Wanasimba kama kuna kitu kinahitajika hata kiwe kinapatikana chini ya bahari tutakifanya ili Simba iende robo fainali. Jumamosi ni kwenda kumalizia kazi. Hatuwezi kushindwa kwenda robo fainali, yani waporipori wamefuzu alafu sisi wenye mashindano tushindwe? Jumamosi saa 1 usiku tunakutana kumaliza kazi," amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad