NGUVU kubwa kwenye soka la Tanzania inahitajika katika kila idara kutokana na maendeleo kuzidi kuonekana kila iitwapo leo. Hili ni kubwa na linapaswa pongezi kwa kuwa kila timu inaonyesha nia ya kufanya kweli.
Ambacho kinapaswa kuwa endelevu ni
kwenye uwekezaji kwenye kila idara hili litaongeza nguvu ya ushindani.
Ushindani ukiongezeka hata thamani ya soka pia inazidi kupanda kila wakati.
Sio kwa timu za wakubwa tu hapana
ni muhimu hata kwenye timu za vijana nako pia nguvu ikawa kubwa hii itaongeza
ushindani na upande wa ligi ya vijana ambayo ni mzizi wa kuwa na wachezaji
wazuri wakati ujao.
Ukweli ni kwamba ngazi ya vijana ni
muhimu kutazamwa kwa ukaribu ili kuongeza nguvu kwa kuwa hawa wanatengenezwa
kwa ajili ya kutumika kesho kitaifa na kimataifa.
Kukiwa na ongezeko la wachezaji
kutoka timu za vijana wakiwa wanapewa nafasi pia kwenye timu za wakubwa
taratibu watazidi kuwa imara kwa ajili ya mashindano makubwa.
Ili kuwa na wachezaji wengi wazawa
ambao watafanya vizuri katika timu ya taifa ya Tanzania ni muhimu kuwa na
sehemu nyingi za kuwatengeneza hasa kwenye timu za ndani.
Ikiwa ni timu chache zitakuwa
zinawekeza nguvu kwenye kuwatengeneza wachezaji vijana hili litakuwa ni gumu
kuwa na wazawa wenye uwezo mkubwa wakati ujao.
Kufanya vizuri kwa timu ya taifa ya
Tanzania kunahitaji uwepo wa mwendelezo wa vijana ambao wanaandaliwa kwa wakati
huu katika mashindano mbalimbali.
Furaha ya vijana kufanya vizuri
kwenye mechi na mashindano ambayo watakuwa wanashiriki italeta furaha kesho
kwenye mashindano ya timu ya taifa ya Tanzania.
Ni muda wa kuongeza nguvu pia
kwenye uwekezaji katika soka la vijana kwenye kila timu hii itafanya wachezaji
wengi wazalishwe kuanzia ngazi ya chini.
Uwekezaji ukiwa mkubwa unatoa fursa
kwa timu kubwa kuwapa nafasi wale wachezaji kutoka ngazi ya vijana kucheza
mechi za kimashindano jambo litakalowaongezea hali ya kujiamini.
Vijana wana uwezo wa kufundishika
na kuendelea kuwa kwenye mwendo bora katika mechi za kitaifa na kimataifa hili
lipo wazi.
Wale ambao watapewa nafasi
pia ni muhimu kujituma kila wakati kuonyesha thamani ya kuaminiwa na
benchi la ufundi katika mechi watakazopewa.
Kila timu ni wakati wake kuendelea
kupambana kutengeneza wachezaji kwenye idara ya vijana nguvu ikiwa kubwa huku
italeta matokeo mazuri.
Ikiwa hivyo hata kwenye mechi za
kimataifa vijana wakiwa wanapewa nafasi watazidi kutambua namna hali ilivyo kwa
kuwa ili uwe bora ni lazima ukutane na wapinzani bora kwa nyakati tofauti.
Kila kitu kinawezekana na muda bado
upo kufanya maandalizi kwa ajili ya kesho bora kwa vijana waliopo nje na ndani
ya timu.
Ukweli ni kwama mchezo wa mpira ni
mchezo wa wazi hauhitaji mambo mengi zaidi ya uwekezaji na kufanya kweli kwenye
mechi za kitaifa na kimataifa.
Vijana wakipewa nafasi wanaweza na
wakiandaliwa kwa wakati huu itakuwa ni faida kubwa kwa kukua soka la Tanzania
ambalo kila leo ushindani wake unazidi kuongezeka.
No comments:
Post a Comment