SIMBA QUEENS WAKOMBA POINTI ZA ALLIANCE GIRLS - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday, 28 January 2024

SIMBA QUEENS WAKOMBA POINTI ZA ALLIANCE GIRLS

 


NYOTA wa Simba Queens, Jentrix Shikangwa amesepa na zawadi ya mpira baada ya kufunga hat trick katika Ligi ya Wanawake Tanzania.


Hat trick hiyo ilipachikwa kipindi cha pili kwenye mchezo dhidi ya Alliance Girls uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Januari 27 2024.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba Queens 7-0 Alliance Girls ambao waliyeyusha pointi tatu ugenini.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wameanza kazi upya ndani ya Ligi ya Wanawake Tanzania.

"Mchezaji wetu Shikangwa amefunga hat trick kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa na tunatambua kwamba huu ni mwanzo. Mashabiki wazidi kuwa pamoja na sisi,".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad