KIKOSI cha Simba kimerejea Dar baada ya kuweka kambi Zanzibar kwa muda ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Ni Machi 29 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa
ambapo kwa sasa hamasa zinaendelea mtaa kwa mtaa kuwahamasisha mashabiki wa
Simba kujitokeza Uwanja wa Mkapa kushuhudia mchezo huo.
Ahmed Ally, Meneje wa Idara ya Habari na
Mawasiliano Simba amesema kuwa Ijumaa kazi ni moja kwa mashabiki kujitokeza
uwanjani kushangilia mwanzo mwisho katika mchezo huo na malengo ni kuona
wanapata ushindi ndani ya dakika 90.
KOCHA APEWA MAJUKUMU MAZITO
Ally amesema kuwa uzoefu alionao kocha wa
timu hiyo ni moja ya sababu itakayoongeza nguvu kwa timu hiyo kuvuka hatua ya
robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na kutinga hatua ya nusu fainali.
Ikumbukwe kwamba Simba hesabu kubwa kwa msimu
huu ni kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kugotea mara kwa mara hatua ya
robo fainali jambo ambalo limewafanya viongozi wa timu hiyo kubainisha kwamba
inatosha.
"Kwa uzoefu na ubora wa kocha Abdelhak
Benchikha tunaamini atatuvuzusha kwenda Nusu Fainali.
Tunaamini kwamba kila kitu kinawezekana na hilo
linatupa nguvu kwa ajili ya kuwa kwenye ushindani mkubwa ambao upo ndani ya
uwanja kwa kuwa kila kitu kinawezekana na muda ni sasa.
“Hakuna
katika dunia hii mtu yoyote wakuwazuia mashabiki wa Simba wanapotaka jambo lao,
tuungane tupige goti tufanye kila linalowezekana ili tutimize malengo yetu.
“Wachezaji ni wasikivu na wanatambua kazi kubwa
inahitajika kufanyika uwanjani hivyo muda ni sasa kuwa kwenye mpango kazi wa
kutafuta ushindi ndani ya uwanja, mashabiki tujitokeze kwa wingi kwani kila
mchezaji anapenda kuona furaha inabaki ndani ya Simba.
ULINZI KUONGEZEWA DOZI
Benchi la ufundi la Simba limebainisha kuwa
makosa ambayo yamekuwa yakifanyika kwenye mechi za ligi yanafanyiwa kazi kwa
umakini ili kuwa na safu imara ya ulinzi kwenye mechi zao wanazocheza kutokana
na ushindani kuwa mkubwa kitaifa na kimataifa.
Kwenye safu ya ulinzi ni Henock Inonga, Che
Malone, Mohmaed Hussein, Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji wanaounda
safu ya ulinzi ya timu hiyo ya Simba ambayo ina kazi kupambana dhidi ya Al
Ahly.
Ipo wazi kwamba ndani ya Ligi Kuu Bara, safu
ya ulinzi ya Simba haijawa kwenye mwendo bora katika mechi zake tofauti na zile
inazocheza kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba
amesema kuwa wanatambua makosa yalipo jambo linalowafanya wafanye kazi kwa
umakini kuelekea kwenye mechi zijazo kwa kuwaongezea wachezaji wao dozi
nyingine.
“Unaona kwenye mechi ambazo tunacheza
tunapata ushindi na wakati mwingine tunawapa ruhusa wapinzani kutufunga huwa
tunaongea na wachezaji na tutaongeza dozi nyingine kwenye uwanja wa mazoezi.
“Kikubwa ni kuwa makini kwa kuwa mchezo wa
mpira ni mchezo wa makosa, kuelekea kwenye mechi zetu zijazo tuna imani
tutakuwa imara hilo linawezekana kutokana na wachezaji kujituma na kutimiza
majukumu yao kwa ushirikiano,”.
Kikosi cha Simba baada ya kucheza mechi 19
ndani ya ligi ni mabao 18 ukuta umeruhusu ikiwa namba moja kwa timu ambazo
zimefungwa mabao mengi ndani ya tatu bora msimu wa 2023/24.
AL AHLY NDANI YA DAR
Kete inayofuata kwa Simba ni Machi 30 2024
itakuwa dhidi ya Al Ahly ambao tayari Machi 27 wameanza mapema safari kwa ajili
ya kuwasili Dar kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.
Mchezo ujao kwa Simba ni wa Ligi ya Mabingwa
Afrika itakuwa dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 29
tayari wapinzani wao wameanza safari kuja Dar wanatarajiwa kuwasili Machi 27
kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea katika mchezo huo.
Kila timu inautazama mchezo huo kwa hesabu
kubwa za kupata ushindi kutokana na ukubwa wa mashindano hayo barani Afrika.
No comments:
Post a Comment