FEISAL SALUM ANA BALAA HUYO - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday 19 March 2024

FEISAL SALUM ANA BALAA HUYO


KIUNGO wa Azam FC Feisal  Salum ni namba moja kwa nyota wenye mabao mengi ndani ya kikosi cha Azam FC akiwa kafikisha mabao 13.

Nyota huyo yupo sawa na kiungo mshambuliaji wa Yanga Aziz KI ambaye naye katupia jumla ya mabao 13 msimu wa 2023/24 ikiwa kila mmoja yupo kwenye ubora wake katika kutimiza majukumu yake.

Safu ya Azam FC kwenye upande wa ushambuliaji ni namba mbili ndani ya timu ambazo zipo tatu bora ikiwa imefunga jumla ya mabao 47 baada ya kucheza jumla ya mechi 21.

Mbali na kuwa na mabao 47 pia timu hiyo imekusanya pointi 47 kwenye msimamo ikiwa namba mbili msimu wa 2023/24 ambao ushindani ni mkubwa tofauti yake na vinara wa ligi ambao ni Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ni pointi tano pekee.

Wakati Azam FC ikiwa nafasi ya pili na mabao yake 47 Yanga wao wapo nafasi ya kwanza wakiwa wamecheza jumla ya mechi 20 pekee kete 10 zimebaki kukamilisha mzunguko wa pili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad