ALI KAMWE ISHU YAKE IPO HIVI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday 25 February 2024

ALI KAMWE ISHU YAKE IPO HIVI


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa Ali Kamwe kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupata changamoto za kiafya ghafla usiku wa Februari 24 2024.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ushindi unaowapeleka moja kwa moja hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Muda mchache kabla ya mchezo huo kugota mwisho, Kamwe alipata changamoto hiyo na kukimbizwa hospitali mapema kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.

Taarifa ambayo imetolewa na Yanga imeweka wazi kuwa kiongozi huyo ambaye anaingia kwenye rekodi ya mashuhuda wa Yanga kutinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika anaendelea vizuri.

"Wananchi, Ofisa habari wetu Ali Kamwe alipata changamoto dakika chache kabla ya mchezo wetu kuisha na kukimbizwa hospitali ya Aga Khan kupata matibabu. Hivi sasa anaendelea vizuri na yuko salama salmin.,".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad