SIMBA KAMILI GADO KUWAKABILI ASEC MIMOSAS - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday 22 February 2024

SIMBA KAMILI GADO KUWAKABILI ASEC MIMOSAS

 


Mikael Igendia Meneja wa Simba amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Ijumaa Simba inakibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapaubao ulisoma Simba 1-1 ASEC Mimosas hivyo waligawaa pointi mojamoja ndani ya kundi B.

Vinara ni ASEC wakiwa na pointi 10 huku Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi tano kibindoni baada ya kucheza mechi 4.

Meneja huyo amesema: "Ni mchezo mgumu ambao tunakwenda kucheza, mazingira yanatupa ruhusa kufanya vizuri kwa kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kutafuta ushindi.

"Kikubwa ni kusubiri muda wa mchezo kwani wachezaji waliopo wapo tayari licha ya wengine kukosekana kutokana na sababu mbalimbali lakini tupo tayari.

"Tutamkosa Ayoub Lakred kutokana na kadi za njano, John Bocco na Willy Onana hawa walipata maumivu lakini wanaendelea vizuri,".


Baadhi ya wachezaji ambao wapo Ivory Coast ni pamoja na Henock Inonga, Clatous Chama, Mzamiru Yassin, Kibu Dennis.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad