UFARANSA na Morocco wanakutana kwa mara ya kwanza kwenye kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia itakayopigwa leo Jumatano kwenye Dimba la Al Bayt huko mjini Al Khor nchini Qatar.
Ufaransa
ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo wanakutana na miamba kutoka Afrika
ambayo imeweka rekodi ya kufikia hatua hiyo kwa mara ya kwanza.
Wababe hao wametinga nusu fainali baada ya kufanya vyema kwenye michezo ya robo fainali. Ufaransa wametinga nusu fainali kwa mara ya saba kwenye michuano hii baada ya kuiondosha England kwa mabao 2-1.
Kwa
upande wao, Morocco imekuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu hatua hii hiyo
ni baada ya kuifunga Ureno bao 1-0 na kuishangaza dunia.
KIKOSI CHA UFARANSA
Licha
ya kikosi chao kukabiliwa na majeraha, Ufaransa wameonekana kuwa na nguvu
katika harakati zao za kutetea ubingwa wao.
Kylian
Mbappe amefanya safu za ulinzi za wapinzani kuwa hofu, hadi sasa amefunga mabao
matano hadi sasa kwenye michuano hiyo, mawili mbele ya washindani wake wa
karibu wanaowania kiatu cha dhahabu.
Ufaransa
wamepoteza mechi moja tu hatua ya makundi kwa bao 1-0 dhidi ya Tunisia ambapo
kocha Didier Deschamps alituma timu B kwa mechi hiyo kwani Les Bleus walikuwa
tayari wamefuzu.
Katika
hatua ya mtoano waliwaondosha Poland kwa mabao 3-1 kabla ya kuibanjua England
2-1 na sasa wako nusu fainali.
KUHUSU MOROCCO
Miamba
hii ya Afrika ilimaliza kinara kwenye kundi lao ambapo walizifunga Ubelgiji na
Canada kabla ya kutoka suluhu na Croatia.
Kwenye
hatua ya 16 Bora Morocco waliushtua ulimwengu kwa kulifunga taifa kubwa kisoka,
Hispania chini ya Kocha wao, Luis Enrique kwa penalti 3-1 katika muda wa ziada.
Ushindi
wa bao 1-0 dhidi ya Ureno kwenye robo fainali ndio umewapeleka nusu fainali na leo
watakuwa na kazi kubwa ya kupambana na kuudhihirishia ulimwengu kuwa timu
kutoka Afrika inaweza kucheza fainali mwaka huu.
VIPI MATOKEO YAO
Hawa
jamaa wamekutana mara 11 kabla ya leo huku Morocco wakishinda mara moja na
Ufaransa mara saba, mechi tatu zikiisha sare.
Hawajawahi
kukutana katika michuano mikubwa na mara ya mwisho kukutana ilikuwa sare ya 2-2
katika mechi ya kirafiki ya kimataifa mwaka 2007.
REKODI YA UFARANSA KOMBE LA DUNIA
Ufaransa
ndio mabingwa watetezi, walishinda mwaka 2018 huko Urusi. Pia walishinda kwenye
uwanja wao wenyewe mwaka wa 1998.
Mwaka
2006 waliibuka washindi wa pili baada ya kufungwa na Italia kwa penalti 5-3,
michuano ilifanyika nchini Ujerumani. Ni nchi mbili pekee - Italia na Brazil -
ambazo zina rekodi ya kushinda taji la Kombe la Dunia mara mbili mfululizo.
REKODI YA MOROCCO KOMBE LA DUNIA
Morocco
imefuzu Kombe la Dunia mara sita lakini haijawahi kufuzu hatua ya 16 Bora.
HALI ZA VIKOSI
Morocco
walimkosa mlinzi wake wa kati Nayef Aguerd, kutokana na jeraha alilopata katika
ushindi wa mikwaju ya penalti kwenye 16 Bora dhidi ya Hispania.
Kwa
upande wao Ufaransa hakuna majeruhi kuelekea mchezo huu.
DONDOO
01:
Olivier Giroud wa Ufaransa amefunga mabao manne kufikia sasa kwenye Kombe la
Dunia la 2022, na atakuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga mabao
matano ndani ya msimu mmoja kwenye michuano hiyo ikiwa leo atatikisa nyavu.
5+
Ufaransa inaweza kuwa timu ya kwanza kuwa na wachezaji wawili waliofunga mabao
matano au zaidi katika Kombe la Dunia kwa msimu mmoja tangu walivyofanya hivyo
Brazil mwaka 2002 (Ronaldo na Rivaldo).
06:Morocco
hawajafungwa katika mechi zao sita zilizopita za Kombe la Dunia (wameshinda 3,
sare 3), ikiwa ni rekodi katika historia ya Kombe la Dunia kwa timu ya Afrika.

No comments:
Post a Comment