Waziri Simai amechukua uamuzi huo kwa kutambua mchango mkubwa Klabu ya Simba katika kutangaza utalii wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla.
Ipo wazi kwamba Klabu ya Simba ilianzisha mkakati wa kuitangaza Zanzibar kupitia kauli mbiu ya Visit Zanzibar katika jezi na mitandao yake ya kijamii wakati huu wa Kombe la Mapinduzi.
Akizungumza kwa niaba ya klabu ya Simba Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amesema,“ Tunaishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutambua mchango wa timu yetu kutangaza utalii hivyo kukuza uchumi wa Zanzibar, tunaona fahari kubwa kuwa sehemu ya maendeleo makubwa Zanzibar inayoyapata.”
Kwenye Mapinduzi 2024 Simba imefanikiwa mpango kazi wa kutinga hatua ya robo fainali ambapo imepangwa kucheza na Jamhuri mchezo unaotarajiwa kuchezwa Januari 8 2024.
No comments:
Post a Comment