Husna Hassani,Dar es Salaam
WANAFUNZI wa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ)
wameutaka uongozi wa serikali ya wanafunzi kuandaa mashindano mengi zaidi ili
kuweza kuibua vipaji .
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Jabir Hamis ambaye ni
mwanafunzi wa ngazi ya cheti alisema kuwa kuna umuhimu wa kuwa na mashindano
mengi zaidi ambayo yanaleta hamasa kwa wengi kuonesha vipaji vyao.
“Ushindani ni kitu kizuri kwani unaibua ujuzi wa kila
mwanafunzi kuweza kupata muda wa kuonyesha kile alicho nacho pamoja na kutoa
fursa kwa wanafunzi kuweza kutambua uwezo wao kimasomo katika kuonesha kile
wanachopenda kufanya “alisema
| Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam wakijipatia chakula katika siku ya tamasha la wanafunzi (Bash) viwanja vya Jangwani See Breeze Dar es Salaam |
.
Shamimu Abel alisema
kuwa kuna kila sababu za uongozi kujali vipaji vya wanafunzi kwa kuwaendeleza
zaidi katika yale wanayojifunza na kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwenye
malengo aliyojiwekea.
Ally Makame ambaye ni naibu waziri wa michezo alisema kuwa
mpango mzima wa kutambua vipaji na matamasha ni mwendelezo ambao utasimamiwa na
serikali ya wanafunzi kwa kushirikiana na uongozi wa chuo kuhakisha kuwa vipaji
vinaibuliwa zaidi.
“Tunatambua umuhimu wa vipaji kwa wanafunzi na maandalizi
zaidi yanafanyika ili kuhakikisha kuwa tunaweza kujua uwezo waliona hiyo ni
kazi tunayoifanya kwa kuwajali wanafunzi wote katika suala zima la
taaluma”alisema
No comments:
Post a Comment