Azam na DSJ hapatoshi leo - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 22 March 2017

Azam na DSJ hapatoshi leo




Na.Jabiri Hamisi,Dar es Salaam
TIMU ya mpira wa miguu ya chuo cha uandishi wa habari Dar Es Salaam (DSJ) inajipanga kulipa kisasi kilicho dumu kwa mwaka mmoja dhidi ya timu ya wanahabari kutoka Azam katika mechi ya Kirafiki itakayopigwa viwanja vya Mabibo.

Kiungo wa timu ya DSJ star (Kulia) Gery Gerad akionesha uwezo kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Azm media na DSJ Star 
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii Naibu waziri wa Michezo DSJ Ally Makame alisema kuwa wamejiaanda kiasi cha kutosha ili kulipa kisasi ambacho kimedumu kwa muda mrefu katika mchezo wa kirafiki.

“Wanahabari wenzentu Azam hivyo sisi ni familia moja waliacha kilio kwetu kwa kutufunga magoli matano tunawakumbuka na uwezo wao tunautambua  wajipange tu kuhakikisha wanabeba mzigo wa kutosha wa magoli “alisema Makame

Vaileth Mawaka mwakilishi kutoka Azam alisema kuwa lengo kubwa la michezo ni kuimarisha ushirikiano na kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata nafasi ya  kuwa mwanafamilia  na kuimarisha mahusiano baina ya wanamichezo.

“Hakuna anayependa kushindwa ila kwetu mchezo ni zaidi ya urafiki kwani inatufanya tuboreshe mahusiano zaidi na kufungua uwanda mpana pamoja na kupata nafasi ya kupumzisha akili kwani muda mwingi tumekuwa tukifanya kazi ya kuhabarisha jamii”alisema Vaileth.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad