MMG wafundwa kuhusu muda - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 20 March 2017

MMG wafundwa kuhusu muda



                                           
Na Mainda Mhando,Dar es Salaam

MKURUGENZI mtendaji  wa Mtaasisi Media Group (MMG) Ambele Mwafulango amewataka wanafunzi kutokukata tamaa katika suala zima la kujifunza na kuhakikisha kuwa wanatumia muda vizuri.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii alisema kuwa siri kubwa ya mafanikio ipo katika kuutawala muda vizuri na kuweka mpangilio wa mambo kwa wakati.


“Mpangilio mzuri wa muda unaleta mafanikio katika kila jambo ni jambo la kuzingatia kwa kila hatua ni lazima kuweka kila kitu katika muda kwani kila kitu kinafanywa ndani ya muda mwafaka kabisa”alisema.
Aliongeza kwa kusema kuwa katika kila jambo la mwanadamu analofanya anategemea kujipanga na kuweka mipango kwa wakati hasa katika suala zima la muda kwa kuwa umakini katika muda unaleta umakini katika utendaji.

Salama Ngale ambaye ni mlezi wa kundi hilo amesema kuwa jambo kubwa la kufanya katika maandalizi ya muda na kuthamini kila jambo ili kuhakikisha kuwa kila jambo linakwenda kwa mpangilio mzuri ili kuhakikisha  kila jambo linakwenda kwa utaratibu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad