DSJ yajipanga kuinua vipaji vya michezo - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 20 March 2017

DSJ yajipanga kuinua vipaji vya michezo



N a Japhary Lesso,Dar es Salaam


Naibu waziri wa wizara ya Michezo wa serikali ya wanafunzi kwa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ) amewataka wanafunzi kutohofia kushiriki kwenye michezo  na mashindano yanayoandaliwa na chuo kwa kuwa ni fursa nzuri kutambua uwezo na vipaji vyao.


Kikosi cha mpira wa miguu DSJ Stars
Akizungumza na mwandishi wa habari hii chuoni hapo alisema kuwa mashindano na michezo inayoandaliwa katika chuo cha uandishi wa habari yana lengo la kuboresha na kuinua vipaji vya
wanafunzi chuoni hapo hivyo kila mmoja anapaswa kuwajitoa.


“Hakuna haja ya kuhofia kuja na aina nyingine ya michezo kwani kila mwanafunzi ana uhuru wa kuchagua na kuandaa michezo anayoipenda tunatoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha kuwa hatuwekezi nguvu nyingi kwenye mchezo wa mpira wa miguu pekee”alisema


Yahaya Jabiri mwanafunzi wa ngazi ya cheti alisema kuwa serikali ya wanafunzi imewekeza nguvu nyingi kwenye mchezo wa mpira wa miguu hali inayofanya kuacha aina nyingine ya michezo kudorora hivyo kuna haja ya kuwekeza kwenye michezo ya aina nyingine pia.


“Wanathamini mchezo wa mpira wa miguu pekee na kushindwa kutoa nafasi kwenye michezo mingine kama vile basketball,riadha pamoja na michezo ya kuvutana kamba hali inayotufanya tushindwe kujifunza michezo mingine kwani inatukosesha fursa ya ajira”alisema


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad