Na.Agnes Mathew,Dar es Salaam
WAZIRI wa elimu kwa serikali ya wanafunzi wa chuo cha
uandishi wa habari Dar es Salaam(DASJOSO) Saitoti Mwalimu amewataka wanafunzi
kushiriki ziara ya kimasomo itakayofanyika mkoani Tanga yenye lengo la kuongeza
ujuzi kwa vitendo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii alisema kuwa kuna
faida kubwa kwa wanafunzi kushiriki kikamilifu ziara ya kimasomo itakayofanyika
mwezi wa nne kwa kuwa watapapata muda mzuri wa kubadili madhari na kuwa ni
watalii wa ndani kwa kutembelea vivutio vya mkoani Tanga.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam(DSJ) |
“Tunatembelea mkoa wa kitalii na wenye upekee itakuwa ni
fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kuweza kutembelea sehemu
mbalimbali ambazo ni za kihistoria pamoja na kutembelea vyombo vya habari
vilivyo mkoani humo kwa muda wa siku nne”alisema.
vilivyo mkoani humo kwa muda wa siku nne”alisema.
Aidha alisema kuwa wanashirikiana na uongozi wa chuo ili
kuhakikisha kuwa lengo la ziara linabaki kuwa la lenye misingi madhubuti na
kusimamia ukweli na uwazi hasa katika matumizi ya fedha na yeyote atakayekiuka
taratibu hatua za kinidhamu zitachukua mkondo wake.
Michel Fredy mwanafunzi wa ngazi ya cheti alisema kuwa kuna
umuhimu kwa wanafunzi kuzingatia taratibu za chuo na kufuata sheria pasipo
kupindisha mambo kwani tabia za kupuuzia huwaponza wengi hali inayopoteza ubora
wa ziara.
pamoja we can
ReplyDeletestudy tour kwa kujifunza zaid