Stashahada yaibuka kidedea kombe la Mbuzi - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday, 12 March 2017

Stashahada yaibuka kidedea kombe la Mbuzi

Na Mercy Julius, Dar es salaam

 

TIMU ya soka ya stashahada muhula wa tatu na wa nne ya chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ) imefanikiwa kutwaa kombe la mbuzi lililohusisha timu tano kutoka madarasa tofauti chuoni hapo.

 

Ushindi huo umekuja baada ya kuigaragaza timu ya ngazi ya cheti kwa goli moja kwa sifuri kwenye mchezo wa fainali uliofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Moyo Dar es Salaam.

Nahodha wa Timu ya ngazi ya Stashahada Gery Gerald (Kushoto) pamoja na Msemaji wa timu hiyo Shukuru Daniel (Kulia) wakipokea zawadi ya Mbuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa walimu chuoni hapo Pro,Victor Sinka (Mwenye shati jeusi) katika viunga vya chuo hicho hivi karibuni  pamoja na Mwalimu wa michezo Deus Malongo na Msaidizi wake Stella Msaliboko.

Akizungumza na MMG Kocha wa timu ya hiyo Haji Mtege alisema kuwa walijipanga vyema tangu awali pamoja na wachezaji kujituma licha ya ugumu uliopatikana kutoka kwa wapinzani 

 

"Mchezo haukuwa rahisi kwetu ila tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kufikia malengo maandalizi mazuri na wachezaji kucheza kwa kushirikiana kumetusaidia kuweza kuwashinda wapinzani wetu hali iliyofanya tukaibuka kidedea"alisema.

 

Dickson Joseph ambaye ni nahodha wa timu ya ngazi ya cheti alisema kuwa wanaimani kubwa na timu yao licha ya kufungwa wanajipanga zaidi kwa ajili ya mashindano mengine ili waweze kufanya vizuri zaidi.

 

"Hatujakata tamaa licha ya kufungwa katika mchezo wa fainali kwani tuna timu nzuri na yenye wachezaji wazuri, bahati haikuwa yetu hali iliyopelekea tukashindwa kuchukua ubingwa hivyo tunajipanga kwa mashindano yajayo "alisema Joseph.






                                                                                                            j

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad