Matokeo yatikisa wanafunzi DSJ - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday, 12 March 2017

Matokeo yatikisa wanafunzi DSJ


WANAFUNZI wametakiwa kuwekeza nguvu katika masomo yao ili waweze kupata matokeo yatakayotoa mwanga kwa wazazi na walezi kuwa na moyo wa kuwagharamia zaidi katika elimu.

Akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho Waziri wa Elimu wa Serikali ya wanafunzi (DASJOSO) Saitoti Mwalimu alisema kuwa ni jukumu la kila mwanafunzi kuhakikisha kuwa anasoma pasipo kukata tamaa.

“Lengo kubwa la mzazi kumpeleka mtoto shule ni kuweza kuona anafikia ndoto zake na kuweza kuihi maisha anyoyataka na sio yale anayoyaweza hivyo kuna ulazima wa kuongeza juhudi katika masomo”alisema Mwalimu.

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari DSJ wakijiandaa na mitihani inayotarajiwa kuanza hivi karibuni

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na MMG Unique  wanafunzi hao,Racheal Kidomo,Patric William,walisema kuwa ya wanafunzi ni kuhakikisha wanafaulu kwenye masomo pamoja na kuongeza ujuzi katika fani ya uandishi .

“Kila mwanafunzi anaishi katika ndoto zake na anaamini kufanya vizuri katika mitihani pamoja na kufanya kazi kwa vitendo ili kuongeza ujuzi zaidi katika tasnia inayohitaji ubunifu kila iitwapo leo”alisema Kidomo.

Patric Wiliam ambaye ni mwanafunzi wa ngazi ya stashada alisema kuwa  matokeo mabaya yanaumiza kwani hakuna anayepanda akitarajia mavuno haba  hivyo kuna umuhimu wa kila mwanafunzi kuzingatia kile anachojifunza na kufanyia kazi. 


    
     

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad