Hapatoshi leo fainali ya BTC na Diploma JK - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 8 March 2017

Hapatoshi leo fainali ya BTC na Diploma JK

JOTO lazidi kupamba moto kwa timu zilizotinga fainali za mashindano ya kombe la mbuzi na kila timu ikijinadi kuibuka na ushindi kabla ya dakika tisini kumalizika.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii kocha wa timu ya wanafunzi wa ngazi ya stashahada Haji Baloe alisema kuwa wachezaji wamejipanga vema kuhakikisha wanashinda michuano hiyo.
"Tumejipanga kushinda na wachezaji wote wapo katika hali nzuri pamoja na mazoezi ambayo yamewaimarisha zaizdi hivyo mbuzi leo wetu"alisema Balou
Faudh Japhary kocha wa timu ya astashahada alisema kuwa mpira ni dakika tisini hawana papara kwani wanajua kile wanachokitaka.
"Ushindi ndio lengo letu kubwa hivyo hakuna haja ya maneno mengi sisi tutawaonesha ustadi wa mpira pamoja na mbinu za kisasa"alisema Japhary

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad