Wanafunzi DSJ wajifunza ziara Chanel ten - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 17 October 2016

Wanafunzi DSJ wajifunza ziara Chanel ten

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ) kwa ngazi ya cheti wamesema kuwa ziara ya masomo katika kituo cha television cha chanel ten imewapa funzo bora linaloongeza ufanisi katika mafunzo yao.
Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es salaam (DSJ) wakiwa wameizunguka meza ya kutangazia ya Channel Ten wakati walipofanya ziara ya kimasomo Ofisini hapo
   Akizungumza na mwandishi wa Mtaasisi   Taris Mlyuka mwanafunzi wa ngazi ya cheti amesema kuwa amejifunza mambo ya msingi ambayo hapo awali hakuyatambua hivyo anapenda ziara ziwepo kwa wanafunzi mara kwa mara.
  "Tumejifunza mpangilio mzima wa habari unavyokuwa na namna habari zinavyohaririwa na kutafutwa kila pande ya Tanzania hivyo tunapenda kuwe na ziara nyingi zaidi ili kutoa fursa kwa wanafunzi kujifunza"Amesema Mlyuka

   Naye Hamisa Semasaba amesema kuwa amefurahi kuweza kujifunza katika kituo cha chanel ten na ameomba uongozi uandae ziara nyingine itakayowapa fursa ya kujifunza zaidi.
    Mwalimu wa somo la habari Fadhil Makenjula amewataka wanafunzi kujifunza zaidi na kuwa wafuatiliaji wa mambo kwa kuwa fani ya uandishi inahitaji umakini katika kufuatilia matukio.
 "Uandishi wa habari ni fani inayohitaji umakini na ufuatiliaji mkubwa wa mambo yanayotokea katika jamii kwa kuwa kazi kubwa ya mwandishi ni kutoa taarifa"amesema

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad