MRATIBU wa masomo wa chuo cha uandishi Dar es Salaam (DSJ)
Joyce Mbogo amesema kuwa jamii inapaswa kufanya tendo la kujitoa kuwa
endelevu na kuwasaidia watoto yatima kwa kuwa uhitaji wao
ni mkubwa na wanahitaji faraja kutoka kwa watu wanaoizunguka jamii .
Mratibu wa masomo DSJ Joyce Mbogo (aliyeshika kichwa) akiwa na Mlezi wa Yatima |
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika kituo cha
watoto yatima cha Msimbazi Center kilichopo ilala jijini Dar es Salaam amesema
kuwa kujitoa ni jambo la kheri na nibudi kuwa hai kwani kunawafanya watu kuwa
karibu na jamii kwa kujitoa kuwatembelea na
kuwafariji pia.
“Tunaishi kwenye jamii nasi pia yatupasa kuwakumbuka wana
jamii wanaotuzunguka kwa kujitoa kuwatembelea na kutoa kile kilicho ndani ya
uwezo wetu kwa kuwa ni jambo jema na linaleta neema kutoka kwa Mungu pamoja na kuongeza upendo wa kweli”.Amesema
Mbogo
Pia ameongeza kwa kusema kuwa watoto wanahitaji kufarijiwa
ili wasijihisi wanyonge kwa kuwa ni taifa la kesho hivyo kuna ulazima wa kuwa
nao karibu zaidi kuwafanya wawe na furaha kila saa kila wakati na wanafarijika
wakiwaona wana jamii wakiwatembelea,.
“Kujitoa kunaleta faraja kwa watoto na uongozi wa chuo na wanafunzi tumejitolea na
miongoni mwa mahitaji muhimu tuliyoleta ni pamojana
sabuni,maziwa,sukari,luku na unga hivyo ni baadhi tu ambavavyo vinahitajika kwa
watoto tunashukuru kwa kuweza kupokelewa na wana Msimbazi”,
Mlezi wa watoto wa kituo cha watoto yatima cha Msimbazi
Center amewashukuru wanafunzi wa DSJ kwa
kuwatembelea na amewataka wazazi wasiwahukumu watoto kwa kuwatelekeza kwa kuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu kupata mtoto.
Akizungumza na
waandishi wa habari kituoni hapo Dada Anna Francis amesema kuwa jamii inabidi
itambue thamani mtoto na kumtuza vyema kwani
makosa yamefanywa na wazazi mtoto hana hatia hivyo hapaswi kupewa adhabu
ya kutelekezwa na wawe na moyo wa kujitolea kuwatunza.
“Jamii inabidi itambue makosa ya kutelekeza yanafanywa na mzazi mwenyewe mtoto hana hatia
hivyo yawapasa kuwatuza wakumbuke kwamba wapo wengine wanaomba usiku na mchana
wapate watoto hivyo kuna haja ya
kuwatunza vema waige mfano kutoka kwa wanafunzi wa DSJ “.Amesema Francis
Pia ameongeza kwa kusema kuwa jamii inabidi ikumbuke
kujitolea kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu
kwani jukumu la kuwalea ni la wana jamii kwa ujumla na kuwachukua watoto endapo
watafuata taratibu.
“Jukumu l a kulea watoto ni letu sote na inaruhusiwa
kuwaasili watoto walotimiza miaka mitatu kwa mzazi ama mlezi anayehitaji endapo
atafuata utaratibu kwa kupitia ustawi wa jamii na kupewa kibali kama atahitaji
kumchukua mtoto wa kumlea ”.
Sostenes Chuma mwanafunzi wa ngazi ya stashahada amesema
kuwa jamii inapaswa ikumbuke kuwatembelea watoto na kujito kuwasaidia kwa kuwa
wakifanya hivyo wanawapa faraja watoto ambao wamekosa mapenzi ya wazazi.
“Inaleta Baraka kutoka kwa Mungu kwa wana jamii ikiwa
watajitolea kuwatembelea watoto na watu walio katika mazingira magumu nawasihi
waige mfano wa wanafunzi kutoka DSJ watakuwa wamefanya kitu kizuri na chenye
maana kwenye jamii”Amesema Chuma
Nana Mzobora mwanafunzi wa ngazi ya stashahada amesemakuwa
anajisikia faraja kuona jamii inasaidia watu walio katika mazingira magumu na
kuwasihi kuwa na moyo huo kwa kuwa jamii inahitaji ushirikiano na kuwasihi
wasichoke kujitoa.
No comments:
Post a Comment