KILE kipengele cha kutamba kuwa ni mkubwa kwa watani za jadi sasa kinapaswa kuonyeshwa kwa vitendo kutokana na mashindani ya kimataifa ambayo yapo mbele yao.
Simba
wao wapo ndani ya Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi na wanatarajiwa kumenyana
na Horoya Februari 11 ugenini na Yanga wao Februari 12 wana kete yao kwenye
Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga
itakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya US Monastri hapa tunakuonyesha baadhi ya vipengele ambavyo wanafanya vizuri ndani ya ligi na
vinapaswa kuonyeshwa anga la kimataifa namna hii:-
Wakali
wa pasi
Ndani
ya Simba wakali wa pasi kwenye ligi wamejaa kila kona ukianzia kwa mabeki
ambapo Mohamed Hussein na Shomary Kapombe hawa wote wametengeneza pasi
tanotano.
Kinara
wa pasi kwa sasa kwenye ligi ni Clatous Chama akiwa nazo kibindoni 14 hii ni
namba kubwa na inaonyesha uwezo wake kuwasoma wachezaji na kuwaelekeza ni
mkubwa basi ni kazi yao kuhamishia yale yote kwenye anga za kimataifa.
Ukiwagusa
Yanga ni Jesus Moloko mwenye pasi nne za mabao anafuatiwa na Aziz KI mwenye
pasi tatu ndani ya ligi ujuzi wao uhamie kwenye anga za kimataifa katika kufanya
kweli.
Mipira
iliyokufa
Chama
na Saidi Ntibanzokiza wanakimbiza kwenye mapigo huru ndani ya Simba huku pasi
zake mbili kwenye mchezo uliopita alizotoa Chama ilikuwa ni kwa mapigo ya faulo
huku Ntibanzokiza yeye akifunga kwa penalti mbele ya Mbeya City.
Yanga
wao wanaye Aziz KI ambaye anawatesa kinomanoma makipa wa Bongo kuanzia Aishi
Manula mpaka Jonathan Nahimana walikutana na balaa lake, pia yupo Djuma Shaban
ambaye ni mtaalamu wa mapigo ya kona.
Balaa
lao ambalo wanalifanya kwenye ligi muda mwingine kwa vitendo kuhamishia kwenye
anga za kimataifa.
Ukuta
chuma
Simba
ni namba mbili kwa timu zilizotunguliwa mabao machache kwenye mechi za ligi
ambayo ni 13 baada ya kucheza mechi 22. Yale makosa ambayo yametokea kwenye
mechi zao ni muhimu kufanyia kazi ili kuwa bora.
Kwa
upande wa Yanga hawa ni namba moja kwa timu iliyotunguliwa mabao machache
ambayo ni 10 ikiwa na ukuta wenye maelewano mazuri ambayo yanahitajika
kuendelea na kwenye mechi za kimataifa.
Watembeza
mikato tahadhari
Mzamiru
Yassin, Ismail Sawadogo, Sadio Kanoute ni miongoni mwa mastaa wanaotembeza
mikato ya kimyakimya na kwenye anga la kimataifa muhimu kuwa na tahadhari ili
kutopata kadi.
Yanga
mkali wao ni Zawad Mauya,Khalid Aucho naye yumo katika kuzidisha ule uimara
wa kupata ushindi ni lazima kuwa makini kwenye ukabaji na kujilinda.
Makipa
kimataifa
Aishi
Manula ana maswali mengi yakujibu hasa kwenye upande wa mapigo huru ambayo
yamekuwa yakimshinda kwenye mechi za hivi karibuni.
Mchezo
uliopita dhidi ya Singida Big Stars alitunguliwa bao kwa pigo la faulo na Bruno
Gomez kazi bado haijaisha kimataifa umakini unahitajika
Djigui
Diarra yupo zake ndani ya Yanga akiwa kwenye ubora ndani ya ligi ambapo mechi 9
mfululizo wakati Yanga ikishinda yeye katunguliwa mabao kwenye mechi moja pekee
dhidi ya Azam FC.
Kujiamini
kwake na kuendeleza ule ubora kwenye anga la kimataifa ni muhimu ili kutimiza
majukumu yake.
Washambuliaji
Juma
Mgunda, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wanatengeneza nafasi
nyingi kwenye mechi zao lakini hawazitumii zote.
Jambo
hili nalo ni muhimu kwa mastaa wa Simba ikiwa ni pamoja na John Bocco, Habib
Kyombo, Jean Baleke kuongeza umakini eneo hilo.
Cedrick
Kaze, kocha msaidizi wa Yanga pia amesema kwenye mechi za
kimataifa nafasi kutengeneza ni ngumu hivyo ikipatikana ni lazima itumike kwa
umakini.
No comments:
Post a Comment