Mpate ni Shida - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 11 October 2016

Mpate ni Shida

MSANII wa filamu anayekuja kwa kasi nchini Tanzania Hassan Mpate amewataka wasanii kujituma zaidi katika kufanya kazi zao za sanaa ili waweze kuendana na kasi ya Rais wa Tanzania John Magufuli.
Msanii wa filamu Hassan Mpate (Aliyeshika simu) akiwa na timu nzima ya Mpate

 Akizungumza na mwandishi wetu Mpate amesema kuwa niwakati kwa wasanii kujitambua na kufanya kazi kwa juhudi ili kufikia malengo na kuendana na sera ya hapa kazi tu.
 "Wasanii wazinduke watambue kuwa nyakati zimebadilika na soko pia
limebadilika ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi kwa juhudi na kwa ari zaidi ili kuendana na uhitaji wa soko la filamu nchini".Amesema Mpate
 Aidha ameongeza kwa kuwataka mashabiki wake kuendelea kumpa sapoti katika kazi zake pamoja na kumkosoa pale anapokosea ili ajifunze zaidi na zaidi katika fani ya uigizaji anayoifanya kwa sasa.
 "Mashabiki wangu nawaomba wasikate tamaa kunipa sapoti pamoja na kutoa maoni yao kwa uwazi ili niweze kutambua wapi nimekosea na wapi niongeze kwa kuwa fani hii ina mambo mengi ambayo ni lazima kujifunza kila siku".Amesema Mpate
  MIongoni mwa filamu alizozicheza Msanii huyo ni pamoja na dunia ya machozi ambayo ipo sokoni pamoja na ndoa za majini ambayo inasambazwa na kampuni ya Steps ltd ya nchini Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad